• HABARI MPYA

  Thursday, September 25, 2014

  LAMPARD APIGA MBILI MAN CITY IKICHAPA MTU 7-0

  MANCHESTER City imesonga mbele katika Kombe la Ligi England, maarufu kama Capital One Cup kufuatia kuichapa mabao 7-0 Sheffield Wednesday usiku huu Uwanja wa Etihad.
  Dakika 45 za kwanza zilimalizika ubao wa matokeo ukisomeka 0-0, lakini dakika ya pili tu ya kipindi cha pili, Frank Lampard akafungua karamu ya mabao. Lamprad alifunga mawili, dakika ya 47 na 90, sawa na Edin Dzeko aliyefunga dakika ya 53 na 77.
  Mabao mengine ya mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England yalifungwa na Yaya Toure dakika ya 60 na kinda Angel Pozo dakika ya 88.
  Kikosi cha Manchester City kilikuwa: Caballero, Sagna, Demichelis, Mangala, Kolarov, Fernandinho/Boyata dk69, Navas, Toure/Pozo dk63, Lampard na Milner/Sinclair dk72, Dzeko.
  Sheffield Wednesday: Kirkland, Buxton, Lees, Zayatte, Mattock, Coke/Dielna dk60, Maguire, Palmer/Helan dk69, Maghoma, May na Madine/Nuhiu dk60.
  Lampard kulia akipongezwa na mchezaji mwenzake baada ya kuifungia Manchester City mabao mawili katika ushindi wa 7-0
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LAMPARD APIGA MBILI MAN CITY IKICHAPA MTU 7-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top