• HABARI MPYA

  Thursday, September 25, 2014

  JERRY SANTO ATUA SAMAIL CLUB, MOMBEKI AMEKIMBIA ‘DILI NJE NJE’ OMAN

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KIUNGO Mkenya, Jerry Santo ameanza ‘mishe’ mpya za kusaka timu ya kuchezea Oman, baada ya mpango wa awali wa kujiunga na Oman Club kushindikana.  
  Jioni ya leo, Santo aliyewahi kuchezea Simba SC na Coastal Union ya Tanga, ametua katika klabu ya Samail kufanya majaribio.
  Wakala Said Maaskary aliyempeleka huko, amesema kwamba kiwango cha Santo kimevutia, lakini tatizo, klabu hiyo ilikuwa inataka zaidi mshambuliaji kuliko kiungo.
  Santo alikwenda huko pamoja na Watanzania wawili, kiungo Athumani Iddi ‘Chuji’ na mshambuliaji Betram Mombeki ambao wao baada ya mipango ya Oman Club kudunda wamerudi nyumbani.
  Jerry Santo akiwa mazozini Samail Club leo

  Wachezaji hao waliitwa na Oman Club kwa ajili ya kusaini mikataba, lakini walipofika huko wakakutana na kikwazo cha kocha ambaye alikuwa tayari ana wachezaji aliotaka wasajiliwe.
  “Nilizungumza nao wote Santo na akina Chuji na Mombeki kwamba wabaki niwatafutie timu nyingine, jana tulikubaliana, ila nashangaa leo wameondoka. Santo kabaki hapa na nimemleta Samail anajaribu bahati yake,”.
  “Ila kama Mombeki angebaki hapa na hawa jamaa walikuwa wanataka mshambuliaji naamini wangemchukua pia,”amesema Maaskari alipozungumza na BIN ZUBEIRY jioni hii.
  Hata hivyo, Maaskary, Mtanzania anayeishi na kufanya kazi Oman akiwa wakala anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), amesema anafanya mpango wa kumrudisha Mombeki nchini humo kwa kuwa Samail inamhitaji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JERRY SANTO ATUA SAMAIL CLUB, MOMBEKI AMEKIMBIA ‘DILI NJE NJE’ OMAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top