• HABARI MPYA

  Sunday, September 28, 2014

  KAGERA SUGAR YAICHAPA 2-0 JKT RUVU CHAMAZI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  KAGERA Sugar imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuilaza mabao 2-0 JKT Ruvu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Mabao ya Kagera Sugar leo yamefungwa na beki wa zamani wa Simba SC, Salum Kanoni Kupela dakika ya 10 kwa penalti na Rashid Mandawa dakika ya 79.
  Ushindi huo wa kwanza katika msimu huu ambao Kagera inaupata ugenini, unafuatia kipigo cha 1-0 kwa Mgambo JKT katika mchezo wa kwanza wa wiki iliyopita Tanga.
  Kwa JKT Ruvu, inakutana na kipigo hicho kwenye Uwanja wa nyumbani, baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana na Mbeya City ugenini, Uwanja wa Sokoine, Mbeya wiki iliyopita.

  Mchezo mwingine wa ligi hiyo uliofanyika leo, Yanga SC imeifunga Prisons ya Mbeya mabao 2-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Mbrazil, Andrey Coutinho na Simon Msuva, wakati la Prisons limefungwa na Ibrahim Kahaka.
  Mechi za jana, Mtibwa Sugar ilishinda 3-1 dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara mabao 3-1 Uwanja wa Manungu Turiani, Morogoro, Mbeya City, ilishinda 1-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga Uwanja wa Sokoine, Mgambo JKT ilifungwa nyumbani bao 1-0 na Stand United ya Shinyanga, Azam FC ilishinda 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani Uwanja wa Azam Complex, wakati Simba SC ililazimishwa sare ya 1-1 na Polisi Morogoro Uwanja wa Taifa.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAICHAPA 2-0 JKT RUVU CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top