• HABARI MPYA

  Tuesday, September 30, 2014

  SIMBA SC YAUNDA SEKRETARIETI MPYA ‘NZITO’

  Na Samira Said, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba SC imetangaza Sekretarieti yake mpya ambayo itakuwa na majukumu ya kiutawala na kuratibu shughuli zote za uendeshaji wa klabu.
  Taarifa iliyotolewa na Rais wa Simba SC, Evans Aveva imesems kwamba Sekretarieti hiyo itakuwa ikifanya kazi zake chini ya kamati ya utendaje ambayo imeundwa na Rais wa klabu, makamu wake na wajumbe wengine wa kuteuliwa na kuchaguliwa kupitia uchaguzi mkuu wa klabu ya simba.
  Ameutaja muundo wa sekretarieti hiyo kuwa ni Katibu Mkuu Stephen Ally, Mhasibu Amos Juma Gahumeni, Ofisa Habari Humphrey Nyasio, Ofisa Operesheni, Stanley Philipo, Ofisa Utawala Hussein Mozzy, pamoja na Mtunza ofisi, Juma Issa Matari. 
  Rais wa Simba SC, Evans Aveva

  Aveva amesema kwamba Sekretarieti hiyo imeshaanza kazi kuanzia Septemba 1, hivyo Kamati ya Utendaji inawaomba wanachama, washabiki na wadau wote wa michezo kuipa sekretarieti hiyo ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa majukumu yake katika klabu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAUNDA SEKRETARIETI MPYA ‘NZITO’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top