• HABARI MPYA

  Sunday, September 28, 2014

  CS SFAXIEN YAPIGWA NJE, NDANI NA KUTUPWA NJE LIGI YA MABINGWA... AS VITA MWAKA HUU NI NOMA!

  Etikiama Agiti wa AS Vita
  TIMU ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imekata tiketi ya kucheza Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 1981 baada ya jana kuifunga CS Sfaxien mabao 2-1 katika Nusu Fainali ya pili.
  Vigogo hao Kinshasa wanasonga mbele katika fainali itakayopigwa Oktoba kwa ushindi wa jumla wa 4-2, baada ya awali kuifunga Sfax kama jana katika mchezo wa kwanza mjini Kinshasa.
  Mabingwa hao wa mwaka 1973 sasa wanasubiri mshindi wa jumla wa Nusu Fainali nyingine ya pili leo mjini Lubumbashi kati ya wenyeji TP Mazembe na ES Setif ya Algeria. Mazembe walifungwa 2-1 katika mchezo wa kwanza na leo wanahtaji ushindi wa 1-0 kuungana na Vita fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CS SFAXIEN YAPIGWA NJE, NDANI NA KUTUPWA NJE LIGI YA MABINGWA... AS VITA MWAKA HUU NI NOMA! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top