• HABARI MPYA

  Saturday, September 27, 2014

  MIEMBENI YATANDIKWA 4-1 NA ZIMAMOTO LIGI KUU ZENJI

  Na Ameir Khalid, ZANZIBAR
  MIEMBENI SC bado haijaweza kuona mwanga wa matumaini katika Ligi Kuu ya soka Zanzibar Grand Malt msimu huu.
  Wakongwe hao waliotoa sare michezo yao miwili ya awali, leo jioni wamesambaratishwa na Zimamoto kwa kipigo kitakatifu cha mabao 4-1 uwanja wa Amaan.
  Ushindi huo wa tatu kwa Zimamoto umeifanya itimize pointi tisa ikiongoza ligi hiyo inayoshirikisha timu 12 Unguja na Pemba.
  Waokozi hao wa majanga walitawala mchezo kwa muda mwingi na kuanza kupachika bao la kwanza dakika ya 13 likifungwa na Khatib Said.
  Wachezaji wa Zimamoto wakishangilia ushindi wa leo

  Hata hivyo, dakika mbili baadae Miembeni walichomoa kwa bao lililowekwa kimiani na Hassan Seif ‘Banda’.
  Mabao mengine ya Zimamoto yalifungwa na Khatib Said tena mnamo dakika ya 31, Ibrahim Hilika dakika ya 58 na Hakim Khamis aliyehitimisha ushindi huo mnono katika dakika ya 83.
  Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa mchezo mmoja katika uwanja wa Amaan utakaozikutanisha timu za Kipanga na Chuoni SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MIEMBENI YATANDIKWA 4-1 NA ZIMAMOTO LIGI KUU ZENJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top