• HABARI MPYA

  Monday, September 22, 2014

  'TANZANIA YAWEZA KUFANYA VIZURI ZAIDI KWENYE SOKA YA WANAWAKE'

  Na Samira Said, DAR ES SALAAM
  VIONGOZI wa soka wanawake wametakiwa kuitumia vyema elimu ya utawala wa mchezo huo wanaoipata kwa sababu kupitia soka la wanawake Tanzania ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa wanayoshiriki.
  Ushauri huo ulitolewa jana na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Sheikh Said Muhammad, wakati akizindua kozi ya utawala wa soka kwa wanawake itakayofanyika kwa muda wa siku tano jijini Dar es Salaam.
  Muhammad alisema kuwa kupitia soka la wanawake Tanzania imeshapiga hatua na endapo viongozi watatumia mafunzo kikamilifu jina la nchi litazidi kutangazika.
  Sheikh Said Muhammad kushoto akiwa na mchezaji wa Yanga SC, Mrisho Ngassa

  Aliwataka viongozi wa soka wanawake wanaoshiriki kozi hiyo iliyoko chini ya Mkufunzi wa Fifa, Henry Tandau, kuhakikisha wanaibua vipaji vya wachezaji wa kike huko mikoani ili kuja kuiimarisha timu ya taifa ya wanawake (Twiga Stars).
  "Onyesheni mfano bora, wanawake mnaweza ila soka ni lazima lianzie chini", alisema Mohammed ambaye pia ni Mwenyekiti wa Azam.
  Naye Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi, alisema kuwa malengo ya kozi hiyo ni kuipa nchi mafanikio kupitia soka la wanawake na shirikisho limejipanga kufanikisha hilo.
  Madadi alisema kuwa endapo TFF itajikita nchi itapata mafanikio.
  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Wanawake TWFA, Rose Kisiwa, alisema kuwa wanafurahia kupata mafunzo hayo kwa sababu uongozi wa sasa ni kutumia taaluma na si uzoefu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: 'TANZANIA YAWEZA KUFANYA VIZURI ZAIDI KWENYE SOKA YA WANAWAKE' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top