• HABARI MPYA

  Monday, September 29, 2014

  AL AHLY ILE ILE ILIYOTOLEWA JASHO NA YANGA SC, YATINGA FAINALI AFRIKA

  VIGOGO wa Misri, Al Ahly wameifunga Coton Sport ya Cameroon mabao 2-1 katika Uwanja wa Kimataifa wa Cairo usiku huu na kiting Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  Mashetani hao Wekundu, ambao walishinda Nusu Fainali ya Kwanza mjini Garoua 1-0 wiki iliyopita, wamefuzu kwa ushindi wa jumla wa 3-1 na sasa watavaana na Sewe Sport ya Ivory Coast katika fainali mwishoni mwa Novemba na mwanzoni mwa Desemba.
  Coton walikuwa wa kwanza kupata bao baada ya Kamilou Daouda kumsetia Jean-Joseph Kombous kumtungua kipa Sherif Ekramy dakika ya 14.
  Kikosi cha Ahly kilichotolewa jasho na Yanga SC katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu, kimetinga Fainali Kombe la Shirikisho

  Al Ahly wangesawazisha mapema dakika ya 37 wakati Amr Gamal alipounganisha kwa kichwa kona, lakini refa wa Zambia, Janny Sikazwe akasema kipa wa Coton alichezewa rafu.
  Lakini dakika tano baadaye, Moussa Yedan akaisawazishia Ahly, kabla ya Gamal kufunga la pili akiuwahi mpira uliookolewa kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Walid Soliman dakika ya 77.
  Ahly iliangukia katika Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa. Ahly ndiyo waliowatoa Yanga SC katika hatua ya 32 Bora kwa penalti baada ya sare ya jumla ya 1-1, kufuatia kila timu kushinda 1-0 nyumbani kwake.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AL AHLY ILE ILE ILIYOTOLEWA JASHO NA YANGA SC, YATINGA FAINALI AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top