• HABARI MPYA

  Monday, September 29, 2014

  KAVUMBANGU ADHIHIRISHA KWELI MKALI WA MABAO, AFUNGA SABA MECHI NANE AZAM FC

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI Didier Kavumbangu amedhihirisha kweli ni mkali wa mabao, baada ya kuifungia klabu yake mpya Azam FC mabao saba ndani ya mechi nane.
  Kati ya mabao hayo, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Burundi, manne amefunga katika mechi mbili tu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kuashiria kwamba yuko tayari kutwaa kiatu cha dhahabu msimu huu.
  “Nimefurahi kufanya vizuri katika mechi hizi mbili, na nitaongeza bidii nifanye vizuri zaidi, kwa sababu hiki ndicho kimenileta hapa, kufanya kazi. Nitafanya kazi. Mimi kufunga ndiyo starehe yangu ya kwanza. Ninaposhangilia bao, huwa nasikia raha sana,”alisema Kavumbangu juzi.
  Didier Kavumbangu kushoto amedhihirisha kweli ni mkali wa mabao baada ya kuifungia Azam FC mabao saba katika mechi nane

  Kavumbangu juzi alifunga mabao yote mawili Azam FC ikishinda 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani katika Ligi Kuu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam wakati kabla ya hapo, katika mchezo wa kwanza, alifunga mabao mawili pia, mabingwa hao wa Bara wakishinda 3-0 dhidi ya Polisi Morogoro. 
  Kavumbangu ametua Azam FC msimu huu akitokea Yanga SC aliyojiunga nayo mwaka 2012 kutoka Atlecito ya kwao Burundi.  
  Na akiwa Yanga SC, ndani ya miaka yake miwili, Kavumbangu alifunga mabao 31 katika mechi 63, akishinda mataji mawil, ubingwa wa Ligi Kuu na Ngao ya Jamii.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAVUMBANGU ADHIHIRISHA KWELI MKALI WA MABAO, AFUNGA SABA MECHI NANE AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top