• HABARI MPYA

  Monday, September 29, 2014

  BEKI YANGA SC ASEMA BILA ‘KUKAZA’ SHUGHULI PEVU MSIMU HUU LIGI KUU

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  BEKI wa Yanga SC, Juma Abdul amesema Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu ni ngumu na wanapaswa ‘kukaza msuli’ ili kutimiza ndoto ya ubingwa.
  Akizungumza baada ya mechi yao ya jana dhidi ya Prisons ya Mbeya, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, beki huyo wa kulia alisema kwamba upinzani walioupata jana kutoka kwa timu hiyo ya jeshi la Magereza ni mkubwa.
  “We jaribu kuangalia, kama Prisons wanacheza hivi mechi ya ugenini, wakiwa huko kwao inakuwaje? Hii maana yake ligi ya mwaka huu ni ngumu,”amesema.
  Beki wa Yanga SC, Juma Abdul amesema Ligi ya msimu huu ngumu

  Abdul amesema kwamba yeye na wachezaji wenzake wote wa Yanga SC wameliona hilo na kuanzia sasa wataongeza bidii katika mechi zijazo.
  “Yaani sasa kila mechi ucheze kama fainali, ukiligeza kidogo tu unapoteza pointi, kitu ambacho si kizuri, nadhani mimi na wachezaji wenzangu tumeliona hilo,”amesema Juma.
  Yanga SC jana ilishinda 2-1 kwa mbinde mbele ya Prisons Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga ilitangulia kupata bao dakika ya 34 mfungaji Andrey Coutinho kabla ya Prisons kusawazisha dakika ya 67 kupitia kwa Ibrahim Kahaka, kabla ya Msuva kufunga la ushindi dakika ya 69.  
  Yanga SC itashuka tena dimbani Oktoba 5, kumenyana na JKT Ruvu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya kuvuna pointi tatu katika mechi mbili za awali.
  Yanga SC ilianza Ligi Kuu kwa kipigo cha ugenini mabao 2-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri Morogoro kabla ya kuokota pointi tatu kwa mbinde mbele ya Prisons jana. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEKI YANGA SC ASEMA BILA ‘KUKAZA’ SHUGHULI PEVU MSIMU HUU LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top