• HABARI MPYA

  Tuesday, September 10, 2019

  AZAM YAMUONGEZEA MKATABA WA MIAKA MIWILI MSHAMBULIAJI WAKE MPYA MUIVORY COAST

  Na Saada Salim, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Azam FC imeingia mkataba mpya wa miaka miwili zaidi na kiungo mshambuliaji, Richard Ella D’jodi kutoka Ivory Coast.
  Djodi amesaini mkataba huo mpya leo mchana mjini Dar es Salaam akiwa sambamba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat'. 
  Mkataba huo utamfanya kuendelea kusalia kwa wababe hao wa Azam Complex kwa miaka mitatu, hadi mwaka 2022.

  Uongozi wa Azam FC umeamua kuingia naye mkataba mpya ndani ya muda mfupi, baada ya Djodi kufanikiwa kuonyesha kiwango kizuri katika mechi mbalimbali za mashindano hali ambayo imemvutia Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije, aliyependekeza kurefushwa zaidi kwa mkataba wake.
  Nyota huyo raia wa Ivory Coast aliyesajiliwa akitokea Ashanti Gold ya Ghana, ambapo hadi sasa katika mechi tatu za mashindano alizoichezea Azam FC amefunga mabao mawili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM YAMUONGEZEA MKATABA WA MIAKA MIWILI MSHAMBULIAJI WAKE MPYA MUIVORY COAST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top