• HABARI MPYA

  Sunday, February 03, 2019

  SAMATTA AFUNGA TENA KRC GENK YASHINDA 2-1 UGENINI LIGI YA UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, BEVEREN
  MSHAMBULIJAI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta usiku wa jana ameifungia bao la kwanza klabu yake, KRC Genk katika ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Waasland-Beveren kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Freethielstadion mjini Beveren.
  Samatta alifunga bao lake hilo dakika ya 59, kabla ya Alejandro Pozuelo Melero kufunga la pili dakika ya 82 kufuatia Boljevic kuanza kuwafungia wenyeji dakika ya 11. 
  Kwa ushindi huo, Genk wanaendelea kuongoza ligi hiyo kwa pointi zao 54, ikifuatiwa na Antwerp yenye pointi 45, baada ya zote kucheza mechi 24.

  Mbwana Samatta (katikati) akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia bao la kwanza Genk katika ushindi wa 2-1 dhidi Waasland-Beveren

  Samatta mwenye umri wa miaka 26, jana amefikisha jumla ya mabao 56 katika mechi 140 za mashindano yote alizoichezea KRC Genk tangu amejiunga nayo Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Kwenye Ligi ya Ubelgiji pekee amefunga mabao 41 katika mechi 108, wakati Europa League amefunga mabao 14 katika mechi 22 na katika Kombe la Ubelgiji amefunga mabao mawili katika mechi tisa.
  Kikosi cha Waasland-Beveren kilikuwa; Roef, Moors, Boljevic, Bizimana, Vanzo/Lulic dk79, Verstraete/Milosevic dk87, Ampomah/Forte dk73, Caufriez, Vukotic, Andrijasevic na Schryvers.
  KRC Genk; Vukovic, De Norre, Dewaest, Aidoo, Maehle, Heynen, Malinovskyi, Pozuelo/Ingvartsen dk89, Ndongala/Paintsil dk59, Trossard na Samatta.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AFUNGA TENA KRC GENK YASHINDA 2-1 UGENINI LIGI YA UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top