• HABARI MPYA

    Wednesday, February 13, 2019

    MANULA ALIVYOKAMILISHA MECHI 70 SIMBA KWA KUWAZUIA AL AHLY DAR

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    ALIKUWA amesimama kwenye lango la Simba kwa mara ya 70 tangu asajiliwa kutoka Azam FC Juni mwaka 2017 na akafanikiwa kuiongoza timu kushinda 1-0.
    Ilikuwa ni katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
    Mechi hiyo ilikuja siku tisa tu tangu Simba SC ichapwe mabao 5-0 na hao hao Al Ahly Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria nchini Misri.
    Wasiwasi ulikuwa ulikuwa mkubwa sana si tu juu ya Simba SC kutofungwa, lakini pia kutoruhusu japo moja dhidi ya mabingwa wa kihistoria wa soka ya Afrika.
    Lakini Aishi akafanya kazi yake vizuri langoni akizuia na kuokoa michomo yote ya hatari iliyoelekezwa langoni mwake, huku mshambuliaji Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere akiifungia Simba bao pekee dakika ya 65.
    Aishi Manula jana amedaka mechi ya 70 tangu asajiliwe Simba SC kutoka Azam FC Juni mwaka 2017 na akafanikiwa kuiongoza timu kushinda 1-0 dhidi ya Al Ahly

    Kwa Simba ilikuwa furaha ya kuendeleza rekodi ya kushinda dhidi ya timu za Kaskazini mwa Afrika katika mechi za nyumbani, lakini pia kufufua matumaini ya kwenda Robo Fainali ya michuano hiyo.
    Ila kwa Aishi Manula, pamoja na furaha ya timu kushinda na sababu zote, lakini pia kwake ilikuwa ni kucheza mechi ya 70 bila kuruhusu bao.
    Hapana shaka mechi 70 ndani ya wastani wa miaka miwili ni kielelezo tosha cha namna Aishi, ambaye pia ni kipa namba moja wa timu ya taifa anavyotumika Simba SC akiwa chachu ya mafanikio ya timu katika misimu hii miwili.
    Mbele na nyuma, kushoto na kulia ni Aishi peke yake – huyo ndiye kipa bora wa Ligi Kuu na nchi kwa ujumla, haijalishi aliruhusu mabao 10 katika mechi mbili mfululizo za ugenini za Simba Kundi D Ligi ya Mabingwa. 
    Uhodari wake ndiyo umeirejesha Simba SC katika ramani ya soka Afrika akianza kwa kuipa ubingwa wa Ligi Kuu kabla ya kuiwezesha kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.
    Katika mechi zote 70 alizodaka Aishi Simba SC, ameruhusu jumla ya mabao 41, akiiongoza timu kushinda mechi 46, kufungwa saba na sare 17.
    Akiwa na umri wa miaka 23 tu, Aishi tayari ameingia kwenye orodha ya makipa bora kuwahi kutokea siyo tu katika klabu yake, Simba bali hata nchini kwa ujumla na sasa anawania kuweka rekodi zaidi ili kuzidi kudhihirisha ubora wake unaomfanya aitwe 'Tanzania One'. 
    Hongera Aishi Salum Manula kwa kufikisha mechi 70 kwa heshima ya kutoruhusu bao dhidi ya Al Ahly.

    Aishi Manula wa tatu kulia waliosimama katika kikosi cha Simba SC kilichoanza jana dhidi ya Al Ahly

    REKODI YA AISHI MANULA SIMBA
    1. Simba 1-0 Rayon Sport (Hakufungwa Kirafiki Simba  Day Taifa)
    2. Simba 0-0 Mlandege FC  (Hakufungwa Kirafiki Amaan, Zbar)
    3. Simba 0-0 (5-4 penalti) Yanga (Hakufungwa Ngao ya Jamii, Taifa Penalti)
    4. Simba 7 – 0 Ruvu Shooting (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
    5. Simba 0 – 0 Azam FC (Hakufungwa Ligi Kuu Chamazi)
    6. Simba 3 – 0 Mwadui (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
    7. Simba 2 – 2 Mbao FC (Alifungwa mbili Ligi Kuu Kirumba, Mwanza)
    8. Simba 0-0 Milambo (Aliingia, hakufungwa Kirafiki A. Mwinyi, Tabora)
    9. Simba 2-1 Stand United (Alifungwa moja Ligi Kuu Shinyanga)
    10. Simba 1 – 1 Mtibwa Sugar (Alifungwa moja Ligi Kuu Uhuru)
    11. Simba 4 – 0 Njombe Mji (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
    12. Simba 1-1 Yanga (Alifungwa moja Ligi Kuu Uhuru)
    13. Simba 1-0 Mbeya City (Hakufungwa Ligi Kuu Sokoine)
    14. Simba 1-0 Tanzania Prisons (Hakufungwa Ligi Kuu Sokoine)
    15. Simba 1-1 Lipuli FC (Alifungwa moja Ligi Kuu Uhuru)
    16. Simba 1-1 (Penalti 3-4) Green Warriors (Alifungwa moja, na penalti nne Kombe la TFF Chamazi)
    17. Simba 2-0 Ndanda FC (Hakufungwa Ligi Kuu Nangwanda)
    18. Simba 4-0 Singida United  (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
    19. Simba 2-0 Kagera Sugar  (Hakufungwa Ligi Kuu Kaitaba)
    20. Simba 4-0 Maji Maji FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
    21. Simba 3-0 Ruvu Shooting FC (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
    22. Simba 1-0 Azam FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
    23. Simba 4-0 Gendarmerie Tnare  (Hakufungwa, Kombe la Shirikiaho Kuu Taifa)
    24. Simba 2-2 Mwadui FC (Alifungwa mbili Ligi Kuu Kambarage)
    25. Simba 1-0 Gendarmerie Tnare  (Hakufungwa – Kombe la Shirikisho Djibouti)
    26. Simba 5-0 Mbao FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
    27. Simba 3-3 Stand United (Alifungwa zote tatu Ligi Kuu Taifa)
    28. Simba 2-2 Al Masry  (Alifungwa mbili moja kwa penalti Kombe la Shirikisho Taifa)
    29. Simba 0-0 Al Masry  (Hakufungwa Kombe la Shirikisho Port Said)
    30. Simba 2-0 Njombe Mji FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa Njombe)
    31. Simba SC 1-0 Mtibwa Sugar (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa) 
    32. Simba 3-1 Mbeya City  (Alifungwa moja Ligi Kuu Taifa)
    33. Simba 2-0 Tanzania Prisons  (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
    34. Simba 1-1 Lipuli FC  (Alifungwa moja, Ligi Kuu Samora)
    35. Simba 1-0 Yanga SC (Hakufungwa, Ligi Kuu Taifa)
    36. Simba 1-0 Ndanda FC  (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
    37. Simba 1-0 Singida United  (Hakufungwa Ligi Kuu Namfua)
    38. Simba 0-0 (3-2 Penalti) Kariobangi Sharks  (Hakufungwa, akaokoa penalty moja SportPesa SuperCup Nakuru)
    39. Simba 0-0 (5-4 Penalti) Kakamega Homeboys (Hakufungwa SportPesa SuperCup Nakuru)
    40. Simba 0-2 Gor Mahia (Alifungwa mbili SportPesa SuperCup Nakuru)
    41. Simba SC 1-1 F.C.E KSAIFA (ya Palestina, hakufungwa kirafiki ziara ya Uturuki)
    42. Simba SC 3-1 MC Oujder (ya Morocco, hakufungwa Kirafiki ziara ya Uturuki)
    43. Simba SC 1-1 Asante Kotoko (ya Ghana, alifungwa moja Kirafiki Simba Day Taifa)
    44. Simba SC 2-1 Arusha United (Alifungwa moja Kirafiki Uwanja wa S.A. Abeid, Arusha)
    45. Simba SC 2-1 Mtibwa Sugar (Alifungwa moja Ngao ya Jamii Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza)
    46. Simba SC 1-0 Tanzania Prisons (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
    47. Simba SC 2-0 Mbeya City (Hakufungwa, Ligi Kuu Taifa alitoka baada ya kuumia dk53 akaingia Ally Salim)
    48. Simba SC 0-0 Ndanda FC (hakufungwa Ligi Kuu Mtwara)
    49. Simba SC 0-1 Mbao FC (Alifungwa moja kwa penalti Ligi Kuu Mwanza)
    50. Simba SC 3-1 Mwadui FC (Alifungwa moja Ligi Kuu Shinyanga)
    51. Simba SC 0-0 Yanga SC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
    52. Simba SC 2-1 African Lyon (Alifungwa moja Ligi Kuu Taifa)
    53. Simba SC 3-0 Stand United (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
    54. Simba SC 5-1 Alliance FC (Alifungwa moja Ligi Kuu Taifa)
    55. Simba SC 5-0 Ruvu Shooting FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
    56. Simba SC 2-0 JKT Tanzania (Hakufungwa Ligi Kuu Mkwakwani)
    57. Simba SC 0-0 Lipuli FC (Hakufungwa Ligi Kuu Uwanja wa Taifa)
    58. Simba SC 4-1 Mbabane Swallows (Alifungwa moja Ligi ya Mabingwa Afrika Taifa)
    59. Simba SC 4-0 Mbabane Swallows (Hakufungwa Ligi ya Mabingwa Afrika Manzini)
    60. Simba SC 1-2 Nkana FC (Alifungwa mbili Ligi ya Mabingwa Afrika Kitwe) 
    61. Simba SC 3-1 Nkana FC (Alifungwa moja Ligi ya Mabingwa Afrika Taifa)
    62. Simba SC 3-0 Singida United (Hakufungwa Ligi Kuu Uwanja wa Taifa)
    63. Simba SC 1-0 KMKM (Hakufungwa Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    64. Simba SC 3-0 JS Saoura (Hakufungwa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Taifa)
    65. Simba SC 0-5 AS Vita (Alifungwa tano Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Kinshasa) 
    66. Simba SC 2-1 AFC Leopards (Alifungwa moja SportPesa Super Cup Taifa)
    67. Simba SC 1-2 Bandari FC (Alifungwa mbili SportPesa Super Cup Taifa)
    68. Simba SC 0-5 Al Ahly (Alifungwa tano Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Cairo)
    69. Simba SC 3-0 Mwadui FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
    70. Simba SC 1-0 Al Ahly (Hakufungwa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Dar)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANULA ALIVYOKAMILISHA MECHI 70 SIMBA KWA KUWAZUIA AL AHLY DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top