• HABARI MPYA

    Friday, February 15, 2019

    KAMATI YA NIDHAMU YA TFF YAMFUNGIA MIEZI MITATU KATIBU WA RHINO RANGERS

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemfungia Katibu Mkuu wa Rhino Rangers, Dickson Mgalike kutojihusisha na soka kwa miezi mitatu na kumtoza faini ya Sh. Milioni 1 kwa tuhuma za kuongoza mashabiki wa timu yake kuwapiga marefa na Kamisaa.
    Mgalike anadaiwa kufanya kosa hilo baada ya mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara dhidi ya Arusha United uliofanyika Februari 2, mwaka huu Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora na ameadhibiwa kwa mujibu wa Kanuni ya 29 (9) ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
    Taarifa ya Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Mario Ndimbo kwa Vyombo vya Habari leo imesema kwamba katika kikao chake Februari 9, mwaka huu chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Kiomoni Kibamba, Kamati pia imeipiga faini ya Sh. 500,000 Rhino Rangers kutokana na vurugu hizo. 

    Ndimbo amesema Rhino Rangers inatakiwa kulipa faini hiyo ndani ya siku 30 kwa kuzingatia Ibara ya 15(3) ya Kanuni za Nidhamu za TFF.
    Naye Mmiliki wa Changanyikeni Rangers FC, Omary Bawazir amepewa Onyo Kali kwa mujibu wa Ibara ya 10(a) ya Kanuni za Nidhamu za TFF baada ya kukiri kuingia uwanjani katika eneo la kuchezea (pitch) wakati wa mechi dhidi ya Cosmopolitan iliyochezwa Februari 2, 2019 Uwanja wa Chuo cha Bandari, Dar es Salaam.
    Hata hivyo, Kamati imeshindwa kumtia hatiani kwa kosa la kumpiga Mwamuzi kutokana na Mlalamikaji kushindwa kuthibitisha tukio hio. 
    Pia Kamati imekazia faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa Changanyikeni Rangers FC iliyotolewa na Kamati ya Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72), na kuwa faini hiyo ilipwe ndani ya siku 30.
    Kiongozi wa Arusha FC, Hassan Issa amepewa Onyo na kutozwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) baada ya kutiwa hatiani kwa kutaka kumpiga Mwamuzi katika mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) dhidi ya Arusha United SC iliyofanyika Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.
    Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Ibara za 10(a) na 15(2) za Kanuni za Nidhamu za TFF. Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, na faini ilipwe ndani ya siku 30.
    Dennis Shemtoi ambaye pia ni Kiongozi wa Arusha FC naye amepewa Onyo na kutozwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) baada ya kutiwa hatiani kwa kutaka kumpiga Mwamuzi katika mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) dhidi ya Arusha United SC iliyofanyika Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.
    Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Ibara za 10(a) na 15(2) za Kanuni za Nidhamu za TFF. Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, na faini ilipwe ndani ya siku 30 kwa mujibu wa Ibara ya 15(3) ya Kanuni za Nidhamu za TFF.
    Kiongozi wa Arusha FC, Bw. Amasha Masenga amepewa Onyo na faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Ibara za 10(a) na 15(2) za Kanuni za Nidhamu za TFF. 
    Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, faini  ilipwe ndani ya siku 30.  Masenga alilalamikiwa na Bodi ya Ligi kwa kutoa lugha chafu kwenye kikao cha maandalizi ya mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) dhidi ya timu ya Dodoma FC.
    Meneja wa Kumuyange FC, Josephat Sinzo amepewa adhabu ya Onyo na faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Ibara za 10(a) na 15(2) za Kanuni za Nidhamu za TFF. Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, faini ilipwe ndani ya siku 30.
    Alilalamikiwa na Bodi ya Ligi kuwa Novemba 11, 2018 katika mehi namba 14 ya Kundi B Ligi Daraja la Pili aliwatolea lugha chafu Msimamizi wa kituo, Mrisho Bukuku pamoja na Mwamuzi.
    Mchezaji Dastani D Lipinga wa Mgambo Shooting amefungiwa mechi tatu na faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 38(7) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, faini ilipwe ndani ya siku 30.
    Alialamikiwa kuwa Januari 13, 2019 kwenye mechi dhidi ya Geita Gold FC alitaka kumpiga mwamuzi baada ya mchezo huo kumalizika.
    Mchezaji Rashid A Shilla wa Mgambo Shooting amefungiwa mechi tatu na faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 38(7) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, faini  ilipwe ndani ya siku 30.
    Alilalamikiwa kuwa Januari 13, 2019 kwenye mechi dhidi ya Geita Gold FC alimpiga kichwa Meneja wa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi wakati timu zinaingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
    Mtunza Vifaa (Kit Man) Alimu Hadji wa Mashujaa FC amefungiwa kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa miezi mitatu (3) na faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(2) ya Ligi Daraja la Kwanza. 
    Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, faini ilipwe ndani ya siku 30.
    Alilalamikiwa kuwa 03/11/2018 katika Uwanja wa Mwakangale, Mbeya akishirikiana na Daktari wa timu yake alivamia uwanja kwenye eneo la kuchezea (pitch) kwa lengo la kutaka kuwapiga waamuzi.
    Daktari Adamu Maftar wa Mashujaa FC amefungiwa kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa miezi mitatu (3) na faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(2) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, na faini ilipwe ndani ya siku 30.
    Alilalamikiwa kuwa 03/11/2018 katika Uwanja wa Mwakangale akishirikiana na Mtunza Vifaa alivamia uwanja eneo la kuchezea (pitch) kwa lengo la kutaka kuwapiga waamuzi.
    Meneja wa Transit Camp, Bw. Moshi Hamisy amefungiwa kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa miezi sita (6) na faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(2) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, na faini ilipwe ndani ya siku 30.
    Alilalamikiwa kuwa tarehe 10/11/2018 katika mechi namba 31, kundi B Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Green Warriors iliyofanyika Uwanja wa Azam Complex aliingia uwanjani na kumsukuma mwamuzi.
    Kocha Msaidizi wa Transit Camp, Thomas Gama amefungiwa kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa miezi mitatu (3) na faini ya sh. 200,000 laki mbili) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(2) ya Ligi Daraja la Kwanza. 
    Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, na faini ilipwe ndani ya siku 30.
    Alilalamikiwa kuwa tarehe 10/11/2018 katika mechi namba 31, kundi B Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Green Warriors iliyofanyika Azam Complex alifanya vurugu kwa kutokubaliana na maamuzi aliyoyatoa mwamuzi wa mchezo.
    Kiongozi wa Transit Camp, Santos Kato amefungiwa kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa miezi mitatu (3) na faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(2)ya Ligi Daraja la Kwanza. 
    Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, faini  ilipwe ndani ya siku 30.
    Alilalamikiwa kuwa tarehe 10/11/2018 katika mechi namba 31, kundi B Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Green Warriors iliyofanyika Azam Complex alianzisha vurugu na kusababisha mchezo kusimamishwa. Baadae alipelekwa jukwaa kuu lakini aliendelea na vurugu hizo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAMATI YA NIDHAMU YA TFF YAMFUNGIA MIEZI MITATU KATIBU WA RHINO RANGERS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top