• HABARI MPYA

    Wednesday, February 13, 2019

    MEDDIE KAGERE APANIA KUWAFUNGA YANGA SC JUMAMOSI UWANJA WA TAIFA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Rwanda, Meddie Kagere amesema anafikiria jinsi ya kuipa ushindi timu yake, Simba SC katika mchezo dhidi ya mahasimu wa jadi, Yanga Jumamosi.
    Yanga watakuwa wenyeji wa Simba SC Jumamosi Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
    Na kuelekea mchezo huo, Kagere amesema kwamba anaafikiria namna ya kuwafunga Yanga siku hiyo katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu, baada ya mechi ya mzunguko wa kwanza kumalizika kwa sare ya 0-0. 

    Meddie Kagere anafikiria jinsi ya kuipa ushindi Simba SC dhidi ya Yanga Jumamosi

    Kagere amesema hayo leo, siku moja tu baada ya kuisaidia Simba SC kushinda 1-0 dhidi ya Al Ahly kwenye mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
    Kagere mwenye asili ya Uganda, aliye katika msimu wake wa kwanza tu Simba SC tangu awasili kutoka Gor Mahia y Kenya, alifunga bao hilo dakika ya 65 kwa shuti la mguu kulia akimalizia pasi ya kichwa ya Nahodha na mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, John Raphael Bocco kufuatia krosi ya beki Zana Coulibaly kutoka Burkina Faso.
    Kwa ushindi huo, Simba SC imefikisha pointi sita baada ya kucheza mechi nne ikipanda kwa nafasi moja hadi ya pili, nyuma ya Al Ahly wenye pointi saba na mbele ya JS Saoura ya Algeria yenye pointi tano na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yenye pointi nne. 
    Simba SC watahamishia makali yao kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara wakimenyana na watani wao wa jadi, Yanga SC Jumamosi kabla ya kusafiri kuwafuata JS Saoura Machi 9 kabla ya kurejea nyumbani kumalizia na AS Vita Machi 16.
    Timu mbili za juu zitaungana na washindi wengine wa makundi A, B na C kwenda Robo Fainali ya michuano hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MEDDIE KAGERE APANIA KUWAFUNGA YANGA SC JUMAMOSI UWANJA WA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top