• HABARI MPYA

    Monday, February 25, 2019

    AZAM FC YAIPIGA RHINO RANGERS 3-0 NA KUTINGA ‘NANE BORA’ KOMBE LA TFF

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Azam FC imekamilisha hatua ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam. 
    Ushindi huo unaokuja siku mbili baada ya Azam FC kumfukuza kocha wake Mkuu, Hans van der Pluijm na Msaidizi wake, Juma Mwambusi, umetokana na mabao ya Mzimbabwe Tafadzwa Kutinyu dakika ya 21, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dakika ya 54 na Obrey Chirwa dakika ya 69.
    Azam FC inakwenda Robo Fainali ikiungana na vigogo, Yanga SC walioifunga Namungo FC  1-0 bao pekee la mshambuliaji wake Mkongo, Heritier Ebenezer Makambo dakika ya 82 jana Uwanja wa Kassim Majaliwa wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

    Mechi nyingine za jana za ASFC, African Lyon iliitoa Mbeya City kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam, wakati Alliance FC iliifunga Dar City 3-0 Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
    Timu nyingine zilizotinga Robo Fainali ni Singida United iliyoitoa Coastal Union, KMC iliyowatoa waliokuwa mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar iliyoitoa Boma FC na Lipuli FC iliyoitoa Dodoma FC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAIPIGA RHINO RANGERS 3-0 NA KUTINGA ‘NANE BORA’ KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top