• HABARI MPYA

    Friday, February 15, 2019

    YANGA SC IMESHINDA ZAIDI YA SIMBA MECHI ZA WATANI MWEZI FEBRUARI

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    NYASI za Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam zinatarajiwa kutimbika kesho kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga.
    Huo utakuwa mchezo wa marudiano msimu huu baada ya timu hizo kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa kwanza uliofanyika Septemba 30, mwaka jana hapo hapo Uwanja wa Taifa.
    Mchezo wa kesho utachezeshwa na refa Hans Mabena kutoka Tanga atakayesaidiwa na washika vibendera Mohammed Mkono na Kassim Mpanga, wakati Heri Sasi atakuwa refa wa akiba wote wa Dar es Salaam.
    Mchezo wa Jumamosi unakuja wakati Yanga SC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 58 za mechi 23, ikiizidi pointi tisa Azam FC inayofuatia katika nafasi ya pili, ingawa ina mechi mbili mkononi, wakati mabingwa watetezi, Simba SC ni wa tatu kwa pointi zao 36 za mechi 15.
    Viingilio katika mchezo wa Jumamosi vinatarajiwa kuwa Sh. 7,000 kwa mzunguko, Sh. 20,000 VIP B na C na Sh. 30,000 kwa VIP A.
    Simba SC itaingia Uwanja wa Taifa kesho ikitokea hoteli ya Sea Scape eneo la Kunduchi mjini Dar es Salaam ikifanya mazoezi Uwanja wa Boko Veterani, wakati Yanga SC ipo mjini Morogoro. 
    Kihistoria kwa mwezi Februari watani wa jadi kesho watakuwa wanakutana kwa mara ya tisa, Yanga ikiwa imeshinda mechi nne, Simba imeshinda mechi mbili na nyingine mbili timu hizo zimetoka sare.
    Nyota ya nani itang’ara Februari ya kesho, tarehe 16 mwaka 2019? Kipyenga cha mwisho cha refa Hans Mabena kitatoa majibu baada ya dakika 90.


    Kiungo wa Simba SC, George Lucas 'Gazza' akitafuta maarifa ya kumpita beki wa Yanga, Kenneth Mkapa Februari 26, mwaka 1994 katika mechi ya Ligi Kuu. Yanga ilishinda 2-0, mabao ya Mohammed Hussein 'Mmachinga' na James Tungaraza 'Boli Zozo' (marehemu) 

    MATOKEO MECHI ZA WATANI MWEZI FEBRUARI
                      P W D L GF GA GD Pts
    Yanga SC 8 4 2 2 10    4 6 14
    Simba SC 8 2 2 4 4 10 -6 8

    ORODHA YA MECHI ZA WATANI MWEZI FEBRUARI
    FEBRUARI 10, 1983 (Ligi Kuu)
    Yanga v Simba.
    0-0
    FEBRUARI 26, 1994(Ligi Kuu)
    Yanga v Simba 
    2-0
    WAFUNGAJI: Mohammed Hussein 'Mmachinga' na James Tungaraza 'Boli Zozo'.
    FEBRUARI 25, 1996 (Ligi Kuu)
    Yanga v Simba
    2-0
    FEBRUARI 21, 1998 (Ligi Kuu)
    Yanga v Simba 
    1-1
    WAFUNGAJI: 
    Yanga: Akida Makunda dk. 46
    Simba: Athumani Machepe dk. 88
    FEBRUARI 10, 2001 (Kombe La Tusker)
    Yanga Vs Simba (fainali) 0-0
    (Simba ilishinda kwa penalti 5-4, Uwanja wa Taifa)
    FEBRUARI 17, 2001 (Ngao Ya Jamii)
    Yangs 2-1 Simba 2-1, Dsm
    WAFUNGAJI: 
    YANGA: Edibilly Lunyamila dk. 47, AllyYussuf 'Tigana' dk 80.
    SIMBA: Steven Mapunda 'Garrincha' dk.43
    FEBRUARI 20, 2016 (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-0 Simba SC
    WAFUNGAJI:
    Donald Ngoma dk39 na Amissi Tambwe dk72
    FEBRUARI 26, 2017 (Ligi Kuu)
    Simba 2-1 Yanga
    WAFUNGAJI:
    YANGA: Simon Msuva (penalti) dk5
    SIMBA: Laudit Mavugo dk66 na Shiza Kichuya dk81
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC IMESHINDA ZAIDI YA SIMBA MECHI ZA WATANI MWEZI FEBRUARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top