• HABARI MPYA

  Saturday, February 02, 2019

  HIGUAIN AFUNGA MAWILI CHELSEA YASHINDA 5-0 ENGLAND

  Mshambuliaji mpya, Gonzalo Higuain akishangilia baada ya kuifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya 16 katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Huddersfield Town kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Stamford Bridge mjini London. Higuain alifunga mawili, lingine dakika ya 69, wakati mengine yamefungwa na Edin Hazard mawili pia, moja kwa penalti dakika ya 45 na ushei na lingine dakika ya 66 huku David Luiz akifunga la tano dakika ya 86.
  Kwa ushindi huo, The Blues inafikisha pointi 50 baada ya kucheza mechi 25, ikirejea nafasi ya nne, mbele ya Arsenal yenye pointi 47 za mechi 24 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HIGUAIN AFUNGA MAWILI CHELSEA YASHINDA 5-0 ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top