• HABARI MPYA

  Saturday, February 02, 2019

  ALLIANCE YAICHAPA LIPULI 2-0 NYAMAGAN NA KUJIINUA TENA LIGI KUUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Alliance FC ya Mwanza leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Lipuli FC ya Iringa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
  Kwa ushindi huo uliotokana na mabao ya Dickson Ambundo dakika ya tisa na Juma Nyange dakika ya 30, Alliance FC inafikisha pointi 31 baada ya kucheza mechi 24 na kupanda hadi nafasi ya saba kutoka ya tisa, wakati Lipuli FC inayobaki na pointi zake 33 za mechi 23, inashika nafasi ya tano.
  Ligi Kuu itaendelea kesho mchezo mmoja tu, mabingwa wa mwaka 1988, Coastal Union wakiwa wenyeji wa vinara, Yanga SC Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kuanzia Saa 10:00 jioni.
  Yanga SC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 53 baada ya kucheza mechi 20, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 47 za mechi 20, KMC pointi 35 za mechi 23, mabingwa watetezi, Simba SC pointi 33 mechi 14 na Lipuli FC pointi 33 mechi 23.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ALLIANCE YAICHAPA LIPULI 2-0 NYAMAGAN NA KUJIINUA TENA LIGI KUUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top