• HABARI MPYA

  Saturday, February 02, 2019

  GAMBO AAHIDI KUJENGA UWANJA WA KISASA ARUSHA KATIKA ENEOLA HEKARI 15

  Na Mwandishi Wetu, ARUSHA
  MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema kwamba wana mpango wa kujenga Uwanja wa kisasa wa Michezo katika eneo la ukubwa wa hekari 15.
  Gambo ameyasema hayo leo asubuhi wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC) mjini Arusha.
  “Serikali ya Mkoa wa Arusha tumetenga hekari 15 kwa ajili ya kujenga uwanja wa kisasa wa michezo na TFF ndiyo watakaousimamia bila kupata usumbufu,”alisema Gambo.
  Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema watajenga Uwanja wa kisasa katika eneo la ukubwa wa hekari 15

  Akifungua mkutano huo, Gambo aliwataka wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kuheshimu mamlaka akisema kuwa hata kama kuna mtu haridhiki na utawala wa sasa wa TFF, hana budi kuiheshimu kwani mamlaka hiyo imewekwa kihalali na inatambuliwa na Serikali.
  “Uchaguzi mlishafanya na tunajua safu ya uongozi ilishakamilika lakini bado kuna watu wanataka kuirudisha TFF ilikotoka. Ombi langu kwenu ni msikubali”, alisema Gambo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GAMBO AAHIDI KUJENGA UWANJA WA KISASA ARUSHA KATIKA ENEOLA HEKARI 15 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top