• HABARI MPYA

  Sunday, July 16, 2017

  SAMATTA AWAFUNGA AJAX WAKITOA SARE 3-3 NA KRC GENK

  Na Mwandishi Wetu, AMSTERDAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amefunga bao timu yake, KRC Genk ikilazimisha sare ya 3-3 ugenini na Ajax katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na msimu.
  Katika mchezo huo uliofanyika bila ya mashabiki Uwanja wa mazoezi wa The Ajax Future, Samatta alifunga bao lake dakika ya 21, akiitoa Genk nyuma kwa 2-1 baada ya Kluivert na Ziyech Ajax kuanza kuifungia Ajax dakika za tatu na 13.
  Trossard akaisawazishia Genk ikawa 2-2 dakika ya 25, kabla ya Neres kuwafungia Ajax bao la tatu dakika ya 56 na Writers kuwasawazishia wageni dakika ya 90 na ushei kwa penalti.
  Mbwana Samatta (kulia) akipongezwa baada ya kuirudisha Genk mchezono kwa bao zuri  
  Mbwana Samatta akimpongeza Trossard baada ya kufunga bao la pili la kusawazisha

  Genk sasa inarejea nyumbani kwenda kuwasubiri Everton ya England kwa mchezo mwingine wa kirafiki kujiandaa na msimu Julai 22 Uwanja wa Luminus Arena, Genk.
  Huu unakuwa mwanzo mzuri wa msimu kwa Samatta, tena akitoka kubadilishiwa jezi kutoka namba 77 hadi 10.
  Na jana Samatta amecheza mechi ya 63 Genk tangu asajiliwe kutoka TP Mazembe ya DRC Januari mwaka jana, akiwa kufunga mabao 23, kati ya hizo ni michezo 41 ndiyo alianza, mechi 21 kati ya hizo alitokea benchi, wakati 12 hakumaliza baada ya kutolewa. 
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa; Jackers, Maehle/Nastic dk18, Brabec/Seigers dk76, Colley/Wouters dk76, Uronen/Khammas dk46, Buffalo/Writers dk60, Berge/Heynen dk66, Trossard/Sabak dk72, Malinovskyi/Zhegrova dk72, Benson/Naranjo dk72 na Samatta/Vanzeir dk76.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AWAFUNGA AJAX WAKITOA SARE 3-3 NA KRC GENK Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top