• HABARI MPYA

    Saturday, July 29, 2017

    KIPA WA TIMU YA TAIFA YA CHAN GHANA ATUA AZAM

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    AZAM FC imejiimarisha baada ya kumsajili kipa Razak Abalora mwenye umri wa miaka 20, kutoka klabu ya WAFA SC ya Ghana kwa mkataba wa miaka mitatu.
    Abalora mwenye rekodi ya kudaka mechi 12 mfululizo bila kuruhusu nyavu zake kuguswa katika mechi 22 msimu huu, anaondoka kwa washindani wa taji la Ligi Kuu ya Ghana baada ya msimu mwingine mzuri kwake.
    Alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ghana ya wachezaji wa nyumbani pekee, inayojiandaa na mchezo ujao wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) dhidi ya Burkina Faso.
    Meneja Mkuu wa Azam FC, Abdul Mohammed (kushoto) akimkabidhi jezi kipa mpya, Razak Abalora kutoka WAFA SC ya kwao, Ghana 

    Na Razak Abalora anaondoka wakati vigogo wa Ghana, Hearts of Oak walikuwa wanajipanga kuzungumza na WAFA ili wamnunue a Razak Abalora.
    Abalora moja kwa moja anakwenda kuwa kipa namba moja wa Azam FC akichukua nafasi ya Aishi Manula anayehamia Simba SC.
    Abalora anakwenda kufanya idadi ya makipa wanne wa kikosi cha kwanza cha Azam, baada ya Mwadini Ali, Benedict Haule na Menata Boniphace. 
    Kuwasili kwa Abalora kunamaanisha Azam italazimika kupunguza mchezaji mmoja wa kigeni ili ibaki na wachezaji saba kwa mujibu wa kanuni, kwani kwa sasa tayari ina Waghana wengine watano, mabeki Daniel Amoah, Yakubu Mohamed, kiungo Enock Atta Agyei na washambuliaji Samuel Afful Yahya Mohammed pamoja na beki wa kushoto Mzimbabwe Bruce Kangwa na kiungo Mcameroon Stephan Kengue.    
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIPA WA TIMU YA TAIFA YA CHAN GHANA ATUA AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top