• HABARI MPYA

    Wednesday, July 26, 2017

    AFRICAN LYON, JKT RUVU ZAPANGWA KUNDI MOJA DARAJA LA KWANZA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU mbili zilizoshuka Daraja kutoka Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita, African Lyon na JKT Ruvu za Dar es Salaam zimepangwa pamoja katika Kundi A Ligi Daraja la Kwanza.
    Kwa mujibu wa orodha ya makundi ya ligi hiyo msimu huu wa 2017 - 2018 iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo, timu nyingine katika kundi hilo hilo ni Ashanti United, Friends Rangers za Dar es Salaam pia, Kiluvya United ya Pwani, Mgambo JKT ya Tanga, Mvuvumwa ya Kigoma na Polisi Moro ya Morogoro.
    Kundi ‘B’ zitakuwa timu za itakuwa na timu za Coastal Union ya Tanga; JKT Mlale ya Ruvuma; KMC ya Dar es Salam, Mawenzi Market ya Morogoro, Mbeya Kwanza ya Mbeya, Mufundi United ya Iringa, Mshikamano na Polisi Dar za Dar es Salaam.
    African Lyon wamepangwa Kundi A pamoja na JKT Ruvu Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara
    Kundi ‘C’ ina timu za Alliance School, Pamba na Toto African za Mwanza, Rhino Rangers ya  Tabora, Polisi Mara ya Mara, Polisi Dodoma ya Dodoma, Transit Camp ya Shinyanga na JKT Oljoro ya Arusha.
    Kadhalika, TFF imeagiza timu za Ashanti United, Friends Rangers, KMC na Polisi Dar ya Dar es Salaam kuwasilisha majina ya viwanja vitakavyotumiwa na timu zao wakati wa ligi hiyo inayotarajiwa kuanza baadaye mwezi ujao.
    Kutaja viwanja hivyo ni matakwa ya Kanuni ya 6 (1) za kanuni Mama ya VPL inayozungumzia Viwanja kadhalika kusomwa pamoja na Kanuni ya 11 inayozungumzia Leseni za Klabu kwamba kila timu haina budi kuwa na viwanja vya mcehi za nyumbani ikiwa ni masharti ya kupata leseni ya klabu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AFRICAN LYON, JKT RUVU ZAPANGWA KUNDI MOJA DARAJA LA KWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top