• HABARI MPYA

    Wednesday, July 26, 2017

    TSHISHIMBI KILA KITU SAFI YANGA, BADO KUSAINI TU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO Papy Kabamba Tshishimbi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), leo amefaulu vipimo mjini Dar es Salaam kuelekea uhamisho wake Yanga SC kutoka Mbabane Swallows ya Swaziland.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, amefanyiwa vipimo hivyo leo katika zahanati ndogo ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya Daktari, Nassor Matuzya.
    Na baada ya kufuzu vipimo hivyo, kiungo sasa anatarajiwa kukaa mezani na viongozi wa Yanga kwa ajili ya kusaini mkataba.
    Yanga ilivutiwa na Tshishimbi baada ya kumuona akiichezea Swallows katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Soka Afrika mapema mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Papy Kabamba Tshishimbi (kushoto) akipongezana na Dk Nassor Matuzya baada ya vipimo vya afya
    Dk Nassor Matuzya akimpima urefu 
    Papy Kabamba Tshishimbi
    Baada ya hapo ikamfuatilia kwenye mchezo wa marudiano Swaziland ambao aliingoza Mbabane Swallows kuichapa Azam 3-0 na kusonga mbele. Tangu hapo, Yanga imekuwa na mawasiliano na mchezaji huyo kwa lengo la kumsajili, ndoto ambazo zinakaribian kutimia.    
    Wakati huo huo kikosi  cha Yanga SC kimeondoka mjini Dar es Salaam jioni ya leo kwenda Morogoro kuweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya.
    Wachezaji 17 tu ndiyo wameondoka leo, ambao ni kipa Youthe Rostand, mabeki Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’. Kevin Yondan, Juma Abdul, Pato Ngonyani, Andrew Vincent ‘Dante’, Mwinyi Mngwali na Abdalla Haji ‘Ninja’. Viungo ni Said Juma ‘Makapu’, Emmanuel Martin, Juma Mahadhi, Geoffrey Mwashiuya, Hussein Akilimali, Pius Buswita na washambuliaji Ibrahim Ajib na Tambwe.
    Wachezaji watano watajiunga na timu baadaye kambini Morogoro, ambao ni makipa Beno Kakolanya na Ramadhan Kabwili, beki Hassan Kessy na Wazimbabwe, kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji Donald Ngoma.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TSHISHIMBI KILA KITU SAFI YANGA, BADO KUSAINI TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top