• HABARI MPYA

    Saturday, July 29, 2017

    SIMBA B YATUPWA NJE KWA MATUTA MICHUANO YA ATF, FAINALI NI YANGA NA PRISONS

    Na Muhiddin Sufiani, MBEYA
    TIMU ya Vijana wa Simba chini ya umri wa miaka 20, jana walishinda kuungana na wenzao wa Yanga katika fainali ya Mechi za Hisani kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI baada ya kufungwa na Tanzania Prisons kwa mikwaju ya penati 6-5 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu wa Sokoine jijini Mbeya.
    Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu zote kutoka uwanjani bila kupata bao, huku timu zote zikicheza kwa taadhari na kufanya mashambulizi ya kushitukiza.
    Katika mchezo huo Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 69 kupitia kwa mshambuliaji wake, Dadi Mbarouk, baada ya kuwatoka mabeki wa Tanzania Prisons Aron Kalambo, aliyekuwa ametoka golini akijaribu kuwahi kumzuia na  kupishana na mpira uliotinga wavuni.
    Mshambuliaji wa Tanzania Prisons B, Mohamed Rashid akimyoka beki wa Simba B, Jacob Jalala (kulia) jana

    Bao la kusawazisha la Tanzania Prisons, lilifungwa na Kassim Hamis, kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 79, baada ya mchezaji wa Simba U20, kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari na kufanya dakika 90 kumalizika timu hizo zikiwa sare kwa kufungana 1-1.
    Baada ya sare hiyo timu hizo zilikwenda katika hatua ya matuta, ambapo zilipigwa jumla ya penati 8, na Tanzania Prisons wakikosa 2 na kupata penati 6 na Simba wakikosa 3 na kupata penati 5.
    Simba wameungana na wenzao Mbeya City Kikosi cha kwanza ambao walitolewa na Kikosi cha Yanga U20 kwa kukubali kichapo cha mabao 3-0 katika mechi hizo za Hisani zilizoandaliwa na Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS, na kushirikisha jumla ya timu Nne za Yanga U20 na Simba U20 kutoka jijini Dar es Salaam, Mbeya City na Tanzania Prisons vikosi vya kwanza Ligi Kuu Bara.
    Mchezo wa fainali unachezwa leo jioni kwenye Uwanja huo wa Sokoine kati ya Yanga U20 na Tanzania Prisons.
    Akizungumzia matokeo hayo Kocha wa Simba U20, Nico Kiondo, alisema kuwa kwa upande wao hali ya hewa ilichangia kwa kiasi kikubwa kupata matokeo hayo lakini pia maandalizi yao hayakuwa ya kutosha kwani wachezaji wengi ni wageni ndani ya Kikosi chao.
    ''Kwa kweli hali ya hewa imetugharimu kupoteza mchezo wa leo lakini pia hatukuwa na mazoezi ya kutosha kabla kwani wachezaji wengi ni wageni waliojiunga na timu msimu huu''. alisema Kiondo
    Kwa upande wake Kocha wa Tanzania Prisons, Abdallah Mohamed, alisemakuwa timu yake imejitahidi kupata matokeo hayo japo imecheza na kikosi cha pili cha Simba kutokana na timu zote kucheza kwa uangalifu kwani hawakuwa na maandalizi ya kutosha baada ya usajili wa wachezaji wapya ambao wengi wao ndiyo walicheza ili kuwajaribu ili kuona mapungufu, huku wengine wakitarajia kucheza katika mchezo wa leo dhidi ya Yanga.
    ''Nimeona mapungufu kwa wachezaji wangu na hasa kwa safu ya ushambuliaji, nitayafanyia kazi ili kupata matokeo mazuri katika mechi zijazo kwani wachezaji wangu wengi ni wageni ambao tumewasajili msimu huu bado hawajazoea hali ya hewa, na wengini nitawajaribu katika mchezo wa leo dhidi ya Yanga''. alisema Mohamed.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA B YATUPWA NJE KWA MATUTA MICHUANO YA ATF, FAINALI NI YANGA NA PRISONS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top