• HABARI MPYA

    Monday, July 24, 2017

    MTIBWA SUGAR YAMSAJILI HASSAN DILUNGA MIAKA MIWILI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO wa zamani wa Yanga SC, Hassan Dilunga amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Mtibwa Sugar ya Turiani, Manungu mkoani Morogoro. 
    Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba, wamevutiwa kipaji cha kuzaliwa cha Dilunga ili kumsajili.
    Katwila, kiungo mshambuliaji wa zamani wa Mtibwa Sugar na timu ya taifa, Taifa Stars, amesema anaamini Dilunga ni mchezaji ambaye ataisaidia timu hiyo.
    Hassan Dilunga akiwa ameshika mkataba wa Mtibwa Sugar baada ya kusiani miaka miwili kuhamishia huduma zake Manungu
    Dilunga anayetokea JKT Ruvu iliyoteremka Daraja baada ya msimu uliopita, ni kati ya wachezaji wawili waliosajiliwa na Mtibwa Sugar mwishoni mwa wiki, mwingine ni mshambuliaji Riffat Hamisi Msuya kutoka Ndanda FC ya Mtwara.
    Na wawili hao wanafanya idadi ya wachezaji wapya waliosajiliwa Mtibwa Sugar kufika sita, baada ya awali mabingwa hao mara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, 1999 na 2000 kuwasajili kipa Shaaban Kado kutoka Mwadui, mabeki Hussein Idd kutoka Oljoro JKT, Salum Kupela Kanoni kutoka Mwadui na kiungo Suleiman Kihimb ‘Chuji’ kutoka Police Moro.
    Lakini Mtibwa Sugar nayo haijaachwa salama katika dirisha hili, kwani baadhi ya wachezaji wake nao wameondoka kwenda timu nyingine, wakiwemo kipa Said Mohammed na mabeki Ally Shomary na Salim Mbonde waliohamia Simba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAMSAJILI HASSAN DILUNGA MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top