• HABARI MPYA

    Saturday, July 29, 2017

    MICHO AACHA KAZI UGANDA, KISA HAJALIPWA MILIONI 140

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mserbia, Milutin Sredojevic ‘Micho’ ameuvunja mkataba na Shirikisho la Soka Uganda (FUFA) kufundisha timu ya taifa ya nchi hiyo, The Cranes kutokana na kutolipwa malimbikizo ya mishahara yake hadi kufika dola za Kimarekani 64, zaidi ya Sh. Milioni 140 za Tanzania. 
    Micho ambaye Septemba 1, mwaka huu atafikisha umri wa miaka 48 ameiambia Bin Zubeiry Sportsv – Online leo kwa simu kutoka Uganda kwamba amelazimika kuondoa The Cranes baada ya uongozi wa FUFA kutothamini mchango wake na kushindwa kumlipa kwa muda mrefu. 
    “Nimevunja mkataba kutokana na kutolipwa mishahara yangu, nimetuma taarifa ya kuvunja mkataba FUFA na kumpa wakala wangu jukumu la kukamilisha taratibu za kuachana nao,”amesema Micho.
    Kocha Mserbia, Milutin Sredojevic 'Micho' akizungumza na Waandishi wa Habari leo 
    Micho anaondoka Uganda baada ya miaka minne, akijivunia kuiwezesha The Cranes kurejea kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) Januari mwaka huu nchini Gabon baada ya miaka 38.
    Kwa ujumla Micho ameiongoza Uganda katika mechi 85, zikiwemo sita za timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 na kati ya hizo 28 za ni kirafiki za kimataifa na 51 ni za mashindano.
    Katika mechi 51 za mashindano, wameshinda mara 29, sare 11 na kufungwa 11, lakini pamoja na mafanikio yote hiyo inasikitisha Micho amekuwa halipwi mishahara.
    Uganda ndiyo nchi ya kwanza Micho kufanya kazi barani Afrika akitokea moja kwa moja kwao, Serbia na kujiunga na klabu ya SC Villa mwaka 2001 alikodumu hadi 2004 alipohamia St. George ya Ethiopia ambako alifundisha hadi mwaka mwaka 2006 alipohamia Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
    Baadaye mwaka huo akaenda kujiunga na Yanga SC ya Tanzania ambako baada ya miezi kadhaa akrudi Ethiopia kufundisha Saint-George hadi 2010 alipohamia Al-Hilal Omdurman ya Sudan alipodumu hadi 2011 alipokwenda kufungua ukurasa mpya taaluma yake, kufundishantimu za taifa akianza na wanda.
    Micho mshindi wa mataji 14 ya Ligi tofauti Afrika, mwaka 2013 aliondoka na Rwanda na kurudi Uganda, alipojiunga na The Cranes ambako aliendeleza mafanikio yake na kujijengea heshima kubwa.
    Haikuwa ajabu baada ya kuiwezesha The Cranes kurudi AFCON kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1978, Micho akaingia kwenye kinyanganyiro cha tuzo ya kocha Bora Afrika, ambayo hata hivyo ilikwenda kwa Pitso Mosimane wa Mamelodi Sundowns, klabu bingwa Afrika, lakini Uganda ikachaguliwa timu bora ya Afrika.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MICHO AACHA KAZI UGANDA, KISA HAJALIPWA MILIONI 140 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top