• HABARI MPYA

    Thursday, July 27, 2017

    MTOTO WA KLUIVERT MIAKA TISA TU ASAINI MKATABA NIKE

    MTOTO wa Patrick Kluivert ameweka rekodi ya mtoto mdogo zaidi Ulaya kusaini mkataba wa nguo na kampuni ya Nike.
    Shane Kluivert, ambaye yumo kwenye vitaabu vya Paris Saint-Germain, amesaini mkataba na kampuni ya nguo za kimichezo akiwa ana umri wa miaka tisa tu.
    Shukrani kwa baba yake, mwanawe wa kiume mdogo, Shane amejipatia umaarufu kwenye mitandao ya kijamii — na Patrick ameposti video zake mitandaoni na picha akicheza.
    Shane sasa amefikisha mashabiki 122,000 wanaomfuatilia Instagram.
    Mtoto wa kiume wa Patrick Kluivert, Shane amesaini mkataba na Nike akiwa ana umri wa miaka tisa tu PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

    Na dalili njema kwake hazionyeshwi na kusainiwa kwake na vigogo wa Ufaransa tu, bali pia kwa kuingia mkataba na kampuni ya vifaa vya michezo ya Marekani — jambo ambalo limemfurahisha sana baba yake, Patrick.
    "Mwanangu ninajivunia sana wewe, Shane Kluivert," ameandika Patrick kwenye Instagram. "Amesaini mkataba wake wa kwanza na Nike akiwa na miaka 9,".
    Kwa upande wake, Shane amedhihirisha furaha yake ya kusaini mkataba huo kwa kuandika: "Najivunia kusaini mkataba wangu wa kwanza na Nike,".
    Makampuni kama Nike na Adidas yanatumia vipaji vinavyojitokeza mapema kama hivi katika shughuli zao.
    Na Shane amesaini mkataba wa 'mwanamichezo mdogo', ambao mara nyingi hupewa vijana wenye umri kuanzia miaka 16 hadi 18 — lakini PSG tayari wanaimiliki silaha hiyo.
    Mtoto mwingine wa Patrick mwenye umri wa miaka 18, Justin pia anafuata nyayo za baba yake baada ya msimu uliopita kupandishwa kikosi cha kwanza cha Ajax.
    Lakini watoto wote hao safari ndefu kufikia mafanikio ya baba yao enzi zake anacheza soka. Enzi zake, Patrick alianzia Ajax kabla ya kwenda kucheza timu kama Barcelona, AC Milan, Newcastle na Sevilla.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTOTO WA KLUIVERT MIAKA TISA TU ASAINI MKATABA NIKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top