• HABARI MPYA

    Thursday, July 27, 2017

    MTIBWA SUGAR WAREJEA MORO KUJIPIMA NA MBEYA CITY

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    BAADA ya kambi ya awali ya wiki mbili mjini Dar esSalaam, klabu ya Mtibwa Sugar inatarajiwa kuondoka kesho kwenda Morogoro kwa ajili ya mchezo maalum wa kuwania Kombe la Faith Baptist Cup utakaofanyika Jumamosi Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
    Mchezo huo ambao huandaliwa na taasisi tatu, hufanyika kila mwaka kwa lengo la kurudisha kilichopatikana katika timu hizi kwa jamii na hii itakuwa mara ya tatu mfululizo, timu hizo zinakutana katika mchezo, huku Mtibwa Sugar wakiwa washindi wa mechi zote mbili zilizopita na Mbeya City safari hii wanataka kufuta uteja.
    Mshambuliaji tegemeo wa Mtibwa Sugar, Stahmili Mbonde akimtoka Nahodha wa Simba, Jonas Mkude msimu uliopita
    Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema; “Kwanza huu mchezo ni muhimu sana kwa Mtibwa Sugar kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, pili mchezo huu ni wa kuwania Kombe, hivyo tunataka tuendeleze kukusanya makombe tofauti tofauti na tatu ni kuwaburudisha wana Morogoro, ambao pia watapata fursa ya kuona baadhi ya nyota waliosajiliwa,”.
    Mtibwa Sugar inakwenda kuivaa Mbeya City ikiwa na wachezaji watano wapya iliyowasajili dirisha hili, kipa Shaaban Kado kutoka Mwadui, mabeki Hussein Idd kutoka Oljoro JKT, Salum Kupela Kanoni kutoka Mwadui na viungo Suleiman Kihimb ‘Chuji’ kutoka Police Moro, Hassan Dilunga kutoka JKT Ruvu iliyoshuka Daraja na mshambuliaji Riffat Hamisi Msuya kutoka Ndanda FC ya Mtwara.
    Mabingwa hao mara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, 1999 na 2000 nao hawajaachwa salama katika dirisha hili, kwani baadhi ya wachezaji wake nao wameondoka kwenda timu nyingine, wakiwemo kipa Said Mohammed na mabeki Ally Shomary na Salim Mbonde waliohamia Simba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTIBWA SUGAR WAREJEA MORO KUJIPIMA NA MBEYA CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top