• HABARI MPYA

    Saturday, July 15, 2017

    RASMI, TIEMOUE BAKAYOKO NI MCHEZAJI MPYA WA CHELSEA

    Kiungo Tiemoue Bakayoko akiwa ameshika jezi ya Chelsea leo baada ya kukamilisha usajili wake kutoka Monaco leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

    WACHEZAJI WALIOTOKA NA KUINGIA CHELSEA HADI SASA 

    WALIOINGIA 
    Tiemoue Bakayoko (Monaco, Pauni Milioni 40); Antonio Rudiger (Roma, Pauni Milioni 31); Willy Caballero (Manchester City, huru); Ethan Ampadu (Exeter City, makubaliano maalum) 
    WALIOONDOKA 
    Nathan Ake (Bournemouth Pauni Milioni 20); Juan Cuadrado (Juventus, Pauni Milioni 17); Asmir Begovic (Bournemouth, Pauni Milioni 10); Bertrand Traore (Lyon Pauni Milioni 8.8); Christian Atsu (Newcastle United, Pauni Milioni 6.2); Nathaniel Chalobah (Watford, Pauni Milioni 6); Dominic Solanke (Liverpool, huru); John Terry (Aston Villa, huru)
    KLABU ya Chelsea imethibitisha kumsajili kiungo Tiemoue Bakayoko kutoka Monaco ya Ufaransa akisiani mkataba wa miaka mitano.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 aliisaidia Monaco kufika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa pamoja na kutwaa taji la Ligue 1 msimu uliopita.
    Chelsea imethibitisha kumsaini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uaransa na kumkabidhi jezi namba 14 atakayokuwa anatumia Uwanja Stamford Bridge.
    Baada ya kusaini, Bakayoko akasema;  "Nina furaha sana kuwa hapa na kujiunga na timu kubwa. Nimekuwa nikiitazama Chelsea. Kusaini ni jambo la kawaida kwangu, kwa sababu ni klabu ambayo niliipenda sana utotoni mwangu,".
    "Sasa ninatazama mbele namna ya kufanya kazi chini ya kocha babu kubwa sambamba na wachezaji wenzangu wakubwa,".
    Bakayoko alipata umaarufu msimu uliopita akiisaidia Monaco kuipiku PSG katika kinyang'anyiro cha taji la Ligi Kuu ya Ufaransa pamoja na kuifunga Manchester City na Borussia Dortmund katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
    Ada ya uhamisho wake kwenda Darajani, inaaminika kuwa Pauni Milioni 40 kwa mchezaji huyo, ambaye anakwenda kucheza pamoja na mchezaji mwenzake katika timu ya taifa ya Ufaransa, N'Golo Kante kutengeneza safu kali zaidi ya kiungo katika Ligi Kuu ya England.
    Wakati Kante ataendelea kuwa mtibuaji wa mipango ya wapinzani na anayetumia nguvu zaidi katika safu ya kiungo, Chelsea itatarajia Bakayoko kuwa mgawaji pasi nzuri na kuutumia mwili vizuri
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RASMI, TIEMOUE BAKAYOKO NI MCHEZAJI MPYA WA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top