• HABARI MPYA

  Monday, August 08, 2016

  YONDAN ARUDI MZIGONI YANGA SC KUELEKEA MECHI NA WAARABU JUMAMOSI TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI tegemeo wa kati wa Yanga, Kevin Patrick Yondan leo ameanza mazoezi na timu yake baada ya kukosekana kwa wiki mbili kutokana na kuwa majeruhi.
  Yondan aliumia wiki mbili zilizopita katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Medeama nchini Ghana, Yanga ikilala 3-1.
  Na baada ya kukosa mchezo wa kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Yanga ikilazimishea sare ya 0-0, Yondan leo amerudi uwanjani.
  Yondan amefanya mazoezi kikamilifu na timu yake leo Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam, kuelekea mchezo wa Jumamosi dhidi ya Mouloudia Olympique Bejaia ya Algeria Kombe la Shirikisho Afrika.
  Kevin Yondan akiwa mazoezini na Yanga Uwanja wa Gymkhana, Dar ees Salaam leo

  Yanga imecheza mechi tano bila kushinda ikilazimishwa sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa kirafiki, ikifungwa 1-0 mara mbili, na Mouloudia Olympique Bejaia nchini Algeria na TP Mazembe Dar es Salaam kabla ya kutoa sare ya 1-1 na Medeama SC mjini hapa na baadaye kwenda kufungwa 3-1 na timu hiyo nchini Ghana katika mchezo wa marudiano.
  Mara ya mwisho Yanga kushinda ilikuwa ni kwenye Fainali ya Kombe la TFF, ilipoibugiza Azam FC 3-1 Uwanja wa Taifa. 
  Yanga itahitimisha mechi zake za Kundi A Kombe la Shirikisho kwa kumenyana na wenyeji TP Mazembe ya DRC mjini Lubumbashi Agosti 23, mwaka huu.
  Mazembe inaongoza Kundi A kwa pointi zake 10 baada ya mechi nne, ikishinda tatu na kutoa sare moja, ikifuatiwa na Bejaia na Medeama, ambazo kila moja ina pointi tano za sare tatu na ushindi mmoja, wakati Yanga inashika mkia kwa pointi yake moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YONDAN ARUDI MZIGONI YANGA SC KUELEKEA MECHI NA WAARABU JUMAMOSI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top