• HABARI MPYA

  Monday, August 08, 2016

  TFF YAIPONGEZA SIMBA SC KWA KUGONGA 'NYUNDO 80'

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeipongeza Klabu ya Simba ya Dar es Salaam kwa kufikisha umri wa miaka 80 tangu kuanzishwa kwake kama ambavyo inaelezwa na viongozi wa sasa wa klabu hiyo.
  Uongozi wa Simba SC kwa takribani miaka saba sasa, wamekuwa wakiazimisha siku ya Agosti 8, kila mwaka wamekuwa na wiki maalumu ya kuweka kumbukumbu ya kuanzishwa klabu hiyo ambako wanachama wao wanafahamu historia ya timu yao.
  Kikosi cha Simba kilichoifunga AFC Leopard 4-0 leo kwenye Simba Day

  TFF tunasema kwamba hicho ni kitu kizuri, ambacho hakina budi kuenziwa kama ambavyo Simba hufanya kwa kushirikiana na jamii hasa kwa kufanya usafi katika mazingira mbalimbali, kutoa zawadi na kufanya ibada za kumbukumbu za waasisi wa klabu hiyo, wachezaji walioichezea Simba na kuipa mafanikio makubwa hususani kwa wale waliotangaulia mbele za haki.
  Wito wetu ni kwamba Uongozi na wanachama wa Klabu ya Simba kuendeleze utamaduni huo wa kuadhikmisha wiki hadi siku ya Simba katika kuenzi historia ya klabu hiyo ambayo ina mchango wake mkubwa kwa soka la Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Kila la kheri Simba Sports Club.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAIPONGEZA SIMBA SC KWA KUGONGA 'NYUNDO 80' Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top