• HABARI MPYA

  Friday, August 19, 2016

  SIMBA YAKAMILISHA UHAMISHO WA MAVUGO, WARUNDI WATOA ITC KIJANA AKIPIGE MSIMBAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imefanikiwa kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo.
  Sifa zimuendee Katibu wa Simba SC, Patrick Kahemele aliyesafiri hadi Bujumbura, Burundi kushughulikia uhamisho wa mkali huyo wa mabao kutoka Vutal’O.
  Kahemele ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwa kifupi tu kwamba; “Nimefanikiwa kupata ITC (Hati ya Uhamisho wa Kimataifa) ya Mavugo na tayari ipo Dar es Salaam, hivyo huyo ni mchezaji wetu halali kuanzia sasa,”alisema Meneja huyo wa zamani wa Azam FC.
  Laudit Mavugo sasa ni mchezaji halali wa Simba SC
  Hadi sasa, Mavugo ameichezea Simba SC mechi mbili za kirafiki ikishinda 4-0 dhidi ya AFC Leopard huku yeye akifunga bao moja na katika sare ya 1-1 na URA ya Uganda, zote Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAKAMILISHA UHAMISHO WA MAVUGO, WARUNDI WATOA ITC KIJANA AKIPIGE MSIMBAZI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top