• HABARI MPYA

  Friday, August 19, 2016

  MALINZI AWAPA POLE MAJIMAJI KUFIWA NA STRAIKA WAO WA ZAMANI KELVIN HAULE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Klabu ya Majimaji ya Songea, mkoani Ruvuma, Humphrey Millanzi kutokana na kifo cha mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Kelvin Haule kilichotokea jana Agosti 18, 2016 kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.
  Rais Malinzi amesema, amepokea taarifa za kifo cha Haule kwa masikitiko makubwa.
  Rais Malinzi amemuelezea Haule kuwa alikuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya timku ya Majimaji ya Songea na Lipuli ya Iringa hivyo ameacha alama ya ucheshi, kujituma na uwajibikaji katika kufanikisha kazi zake katika timu ambazo alichezea.
  Salamu za rambirambi za Rais wa TFF Malinzi pia zimekwenda kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na moyo wa subira wakati huu mgumu wa msiba wa Kelvin Haule.
  Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu Kelvin Haule mahala pema peponi. Bwana alitoa, Bwana alitoa, jina la Bwana lihimidiwe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MALINZI AWAPA POLE MAJIMAJI KUFIWA NA STRAIKA WAO WA ZAMANI KELVIN HAULE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top