• HABARI MPYA

  Tuesday, August 16, 2016

  KAHEMELE AENDA BUJUMBURA KUSHUGHULIKIA UHAMISHO WA MAVUGO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KATIBU wa Simba SC, Patrick Kahemele yuko mjini Bujumbura, Burundi tangu jana kushughulikia uhamisho wa mshambuliaji wao, Laudit Mavugo.
  Akizungumza na Lete Raha leo, Kahemele Meneja wa zamani wa Azam FC, alisema kwamba amekwenda 
  Bujumbura kushughulikia uhamisho wa Mavugo ili awahi kucheza mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC.
  Katibu wa Simba SC, Patrick Kahemele (kulia) akiwa na Rais wa klabu, Evans Aveva (kushoto)
  Mavugo amekuja Simba SC baada ya kumaliza Mkataba wake Vital’O ya kwao Burundi, lakini ajabu klabu hiyo imeibuka na kudai mshambuliaji huyo wa Int’amba Murugamba ana mwaka mmoja zaidi.
  Vital'O inaitaka Simba SC mezani wazungumze biashara ya Mavugo, lakini Kahemele amesema; “Sisi hatuna suala la kuzungumza na Vital’O kuhusu Mavugo. Tunashughulikia uhamisho wake tu kwa wahusika,”.
  Pamoja na hayo, klabu ya Solidarity nayo imeibua madai ya kummiliki Mavugo na kuitaka Simba SC ikao nao mezani kuzungumzia uhamisho wake.
  Hadi sasa, Mavugo ameichezea Simba SC mechi mbili za kirafiki ikishinda 4-0 dhidi ya AFC Leopard huku yeye akifunga bao moja na katika sare ya 1-1 na URA ya Uganda Jumapili, zote Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAHEMELE AENDA BUJUMBURA KUSHUGHULIKIA UHAMISHO WA MAVUGO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top