• HABARI MPYA

  Tuesday, August 16, 2016

  YONDAN AIBUKA MAZOEZINI YANGA KUWAPASHIA AZAM MECHI YA NGAO KESHO

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KAMBI ya Yanga SC imepokea habari njema kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Nazo ni mmoja wa wachezaji wake majeruhi watano, beki wa kati, Kevin Patrick Yondan kufanya mazoezi leo Uwanja wa Gymkhana.
  Majeruhi wengine Yanga ni kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ anayesumbuliwa na maumivu ya kifundo mguu, mabeki Juma Abdul, Andrew Vincent ‘Dante’ wanaosumbuliwa na maumivu ya miguu na kiungo Obrey Chirwa anayeumwa goti.
  Kevin Yondan amefanya mazoezi leo Yanga Uwanja wa Gymkhana

  Kikosi cha kimeendelea na mazoezi leo Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa Ngao dhidi ya Azam Jumatano, kuashiria kupenuliwa kwa pazia la msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Faraja zaidi ni kwamba mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma aliyekuwa majeruhi na akakosa mchezo wa kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar alianza mazoezi jana.
  Ngoma jana alifanya mazoezi kikamilifu Gymkhana kuashiria kwamba anaweza kucheza dhidi ya Azam FC kesho.
  Tayari Yanga imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kufuatia wenyeji Medeama SC kushinda 3-2 dhidi ya TP Mazembe ya DRC juzi katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa Essipong Sports mjini Takoradi, Ghana.
  Kwa matokeo hayo, Medeama watakwenda Algeria kupigania sare kwenye mchezo wa mwisho na wenyeji Mouloudia Olympique Bejaia Agosti 23 ili kwenda Nusu Fainali, siku ambayo Yanga itakuwa ikikamilisha ratiba na TP Mazembe mjini Lubumbashi. 
  Mazembe inaendelea kuongoza Kundi A kwa pointi zake 10 baada ya mechi tano, ikishinda tatu, kufungwa moja leo na sare moja, ikifuatiwa na Medeama yenye point inane, Bejaia pointi tano na Yanga inashika mkia kwa pointi zake nne. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YONDAN AIBUKA MAZOEZINI YANGA KUWAPASHIA AZAM MECHI YA NGAO KESHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top