• HABARI MPYA

    Tuesday, August 16, 2016

    MALINZI ATETEA KITI CHAKE KAGERA, ASHINDA KWA KISHINDO KRFA

    Na Mwandishi Wetu, BUKOBA
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi juzi amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka Kagera (KRFA), baada ya kupata kura 21 kati ya 22.
    Katika uchaguzi huo uliofanyika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Optima, Bananzi, wilayani Misenyi, Salum Chama alitetea nafasi yake ya Katibu Mkuu KRFA kwa kupata kura zote 22, wakati Pelegrinius Rutahyugwa alitetea Ujumbe Mkutano Mkuu waTFF kwa kupata kura zote pia 22.
    Jamal Malinzi (katikati) na safu yake nzima ya uongozi wa KRFA
    Naye Didas Zimbihile alitetea nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu Klabu wa TFF kwa kukusanya kura zote 22.
    Malinzi amekuwa Mwenyekiti wa KRFA tangu Machi 17, mwaka 2012 na katika kipindi chake cha kuwa madarakani amesaidia kwa kiasi kikubwa kurejesha hamasa ya soka kimkoa na sasa mpira wa miguu unachezwa Kagera nzima tena. 
    Aidha, Malinzi amesaidia ukarabati wa Uwanja wa Kaitaba ambaao sasa una mwonekano mzuri ukiwa unapambwa na nyasi bandia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI ATETEA KITI CHAKE KAGERA, ASHINDA KWA KISHINDO KRFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top