• HABARI MPYA

  Sunday, August 07, 2016

  PELE KUMUHAMISHIA MWANAWE WEST HAM

  BABA  wa mshambuliaji wa Swansea City, Andre Ayew, Abedi Pele ambaye pia ni wakala wa mwanawe huyo, amewasili London kumalizia mpango wa mchezaji huyo kuhamia West Ham United.
  Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana yuko mbioni kuhama baada ya klabu hizo mbili kufikia makubaliano juu ya uhamisho huo.
  Timu hizo mbili zimekubaliana uhamisho wa Pauni Milioni 20 kwa Ayew kuondoka Swansea kuhamia West Ham na Abedi Pele, Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika mara tatu, ambaye pia ni baba wa mchezaji huyo wa Swansea, ametua London wiki hii kushughulikia uhamisho huo.

  Abedi Pele (kushoto) akiwa na Andrew Ayew wakati anahamia Swansea kutoka Marseille

  Mchezaji huyo alitua timu hiyo ya Wales kama mchezaji huur msimu uliopita kutoka Marseille ya Ufaransa na mara moja akajipatia umaafufu katika Ligi Kuu ya England baada ya kufunga bao lake la kwanza katika mechi dhidi ya Chelsea.
  Alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Englamd mwezi Agosti baada  ya kazi yake nzuri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PELE KUMUHAMISHIA MWANAWE WEST HAM Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top