• HABARI MPYA

  Monday, January 04, 2016

  YANGA SC YATUMA JINA LA NIYONZIMA CAF

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  JINA la Haruna Niyonzima ni miongoni mwa majina 24 ya wachezaji wa Yanga SC yaliyotumwa Shirikisho la Soka Africa (CAF) kwa ajili ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Pamoja na Yanga SC kutangaza kuvunja Mkataba na Haruna – lakini hakuna hatua zaidi ilizochukua kuashiria kwamba huo ni uamuzi wa dhati, ikiwemo kumpa barua mchezaji mwenyewe kumfahamisha juu ya uamuzi huo.
  Tayari Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema halijapewa taarifa yoyote ya maandishi na Yanga SC juu ya uamuzi wa kuvunja Mkataba na Haruna.
  Majina yaliyotumwa na Yanga SC CAF ni makipa; Ally Mustapha ‘Barthez’, Deogratius Munishi ‘Dida’ na Benedict Tinocco.
  Jina la Haruna Niyonzima limetumwa CAF acheze Ligi ya Mabingwa Afrika

  Mabeki; Nadir Haroub ‘Cannavaro, Kevin Yondan, Mwinyi Hajji, Pato Ngonyani, Vincent Bossou, Juma Abdul, Mbuyu Twite na Oscar Joshua, wakati viungo ni Haruna Niyonzima, Thabani Kamusoko, Said Juma, Salum Telela.
  Washambuliaji ni Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Simon Msuva, Godfrey Mwashiuya, Paul Nonga, Malimi Busungu, Issoufou Boubakar, Matheo Anthony na Deus Kaseke.
  Wiki iliyopita, Yanga SC ilitangaza kuvunja Mkataba na kiungo wake, Haruna Niyonzima kwa madai kwamba kwa kipindi kirefu mchezaji huyo amekuwa akifanya mambo na kuonyesha tabia ambazo si za kianamichezo, gandamizi na ambazo zanaiathiri timu. 
  Ilidai Haruna amekuwa akirudia mambo hayo, licha ya klabu kumuonya mara kadhaa kwa barua na wakati mwingine kumkata mshahara na kwamba tabia zake zimekuwa zikiigharimu timu na klabu.
  Katika ufafanuzi wao, Yanga wamedai Haruna akichelewa na kukosekana mara kwa mara katika programu za timu, hususani anapokuwa amekwenda likizo au kutumikia timu yake ya Taifa ya Rwanda, ambako mara zote amekuwa akiondoka bila hata klabu kupata taarifa au kuombwa ruhusa. 
  Imemtuhumu pia kushiriki katika mashindano ambayo sio rasmi na bila kuruhusiwa na klabu, tu akiweka maslahi yake mbele na sio yale ya klabu.
  Kutokana na mambo haya manne, Yanga imedai Haruna ameshindwa kuishi kwa kufuata vipengele vya Mkataba wake kwa kushindwa kuthamini kazi yake na utovu wa nidhamu kwa programu za Yanga hususani mazoezi ya maandalizi.
  Aidha, Yanga SC imemtaka Haruna kulipa dola za Kimarekani 71,175 (Milioni 143)  kama gharama za kuvunja Mkataba na kwamba itapiga usajili wake popote bila kulipwa fedha hizo. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YATUMA JINA LA NIYONZIMA CAF Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top