• HABARI MPYA

    Saturday, January 09, 2016

    PETER MANYIKA AFIKISHA MECHI 19 ZA KUDAKA BILA KURUHUSU BAO TANGU ATUE SIMBA SC

    REKODI YA PETER MANYIKA SIMBA SC
    Mechi alizodaka 37
    Kutofungwa 19
    Mabao ya kufungwa 29
    MECHI ALIZODAKA PETER MANYIKA SIMBA SC
    Simba SC 0-0 Orlando Pirates (kirafiki aliingia dk43 hakufungwa, Afrika Kusini) 
    Simba SC 2-4 Bidvest Witss (Kirafiki, alifungwa nne Afrika Kusini) 
    Simba SC 0-2 Jomo Cossmos (Kirafiki, alifungwa mbili Afrika Kusini) 
    Simba SC 0-0 Yanga SC (Ligi Kuu, hakufungwa)
    Simba SC 1-1 Prisons (Ligi Kuu, alifungwa moja)
    Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu, aliokoa penalti, akafungwa moja)
    Simba SC 0-0 Express Uganda (Kirafiki, hakufungwa) 
    Simba SC 0-1 Mtibwa Sugar (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar alifungwa moja)
    Simba SC 1-0 Mafunzo (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar hakufungwa)
    Simba SC 1-0 JKU (Kombe la Mapinduzi, hakufungwa)
    Simba SC 4-0 Taifa Jang’ombe (Robo Fainali Kombe la Mapinduzi, hakufungwa)
    Simba SC 1-0 Polisi (Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi, hakufungwa)
    Simba SC 0-0 Mtibwa (Hakufungwa, akampisha Ivo Mapunda dakika ya 90, Simba ikashinda penalti 4-3 Fainali Mapinduzi)
    Simba SC 2-0 Ndanda FC (Ligi Kuu Mtwara, hakufungwa)
    Simba SC 1-1 Azam FC (Ligi Kuu, alifungwa moja) 
    Simba SC 1-2 Mbeya City (Ligi Kuu Taifa, alifungwa mbili)
    Simba SC 2-0 Polisi Moro (Ligi Kuu, aliingia kipindi cha kwanza Ivo alipoumia, hakufungwa) 
    Simba SC 0-2 Mgambo Shooting (Ligi Kuu, alifungwa moja baada ya kuchukua nafasi ya Ivo aliyetolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili)
    Simba SC 3-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu, hakufungwa)
    Simba SC 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu, alifungwa moja)
    Simba SC 3-0 Toto Africans (Kirafiki Mwanza, akiingia kipindi cha pili hakufungwa)
    Simba SC 0-2 Mbeya City (Alifungwa mbili, Ligi Kuu)
    Simba SC 2-1 Zanzibar Kombaini (Alifungwa moja, Kirafiki Zanzibar) 
    Simba SC 4-0 Black Sailor (Hakufungwa Kirafiki Zanzibar)
    Simba SC 3-2 KMKM (Alifungwa mbili, akatolewa kipindi cha pili kirafiki Zanzibar)
    Simba SC 2-1 URA (Alifungwa moja, kirafiki Taifa)
    Simba SC 0-0 Mwadui FC (Hakufungwa, kirafiki Dar alimpokea Dennis Richard)
    Simba SC 3-1 JKU (Alifungwa moja, Kirafiki Zanzibar)
    Simba SC 1-0 African Sports (Hakufungwa, Ligi Kuu Tanga)
    Simba SC 2-0 JKT Mgambo (Hakufungwa, Ligi Kuu Tanga)
    Simba SC 3-1 Kagera Sugar (Alifungwa moja, Ligi Kuu)
    Simba SC 0-2 Yanga SC (Alifungwa mbili, Ligi Kuu Bara)
    Simba SC 1-0 Stand United (Hakufungwa Ligi Kuu)
    Simba SC 1-3 Geita Gold Mine (Alifungwa tatu kirafiki Geita)
    Simba SC 2-2 Jamhuri FC (Alifungwa mbili, Kombe la Mapinduzi)
    Simba SC 1-0 URA FC (Hakufungwa, Kombe la Mapinduzi)
    Simba SC 1-0 JKU FC (Hakufungwa, Kombe la Mapinduzi)
    Peter Manyika amefikisha mechi 19 za kudaka bila kufungwa tangu ajiunge na Simba SC msimu uliopita

    Na Mahmoud Zubeiry, ZANZIBAR
    KIPA chipukizi wa Simba SC, Peter Manyika jana amemaliza dakika 90 bila kuruhusu nyavu zake kuguswa kwa mara ya pili mfululizo katika michuano ya Kombe la Mapinduzi.
    Manyika aliyekuwa langoni SImba SC ikishinda 1-0 katika mchezo huo wa Kundi B jana usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar sasa anafikisha jumla ya mechi 19 za kudaka bila kufungwa kati ya 37 alizocheza.
    Na katika mechi zote 37, Manyika amefungwa mabao 29 tu huku akijiweka katika mazingira mazuri ya kuendelea kudaka na kwenye Nusu Fainali dhidi ya Mtibwa Sugar kesho, baada ya kutofungwa katika mechi mbili mfululizo.
    Mtoto huyo wa kipa wa zamani wa Yanga SC, Manyika Peter alidaka katika sare ya 2-2 na Jamhuri ya Pemba mchezo wa kwanza wa Kundi A, kabla ya kurudi tena katika mchezo dhidi ya URA, timu yake ikishinda 1-0 sawa na jana dhidi ya JKU.
    Kocha Muingereza, Dylan Kerr anaonekana kuanza kujenga tena imani na Manyika baada ya kuimarika kwa kiwango cha kipa huyo siku za karibuni.
    Na tatizo kubwa lililoyumbisha kiwango cha Manyika siku za karibuni ni kipa huyo kutofanya mazoezi ipasavyo.
    Kocha wa makipa, Mkenya Rama Salim alikuwa anamlalamikia Peter Manyika licha ya kuwa kipa bora kuliko wote kikosini, lakini uvivu wa mazoezi unamfanya asiwe katika kiwango kizuri.
    Alisema Manyika ana mwili ambao akizembea mazoezi wiki moja tu anakuwa bonge – na ndiko alikoanza kuelekea siku za karibuni.
    Lakini taratibu Manyika ameanza kurudi katika umbo zuri kiuchezaji baada ya kuongeza juhudi za mazoezi na sasa anaaminika tena, kiasi cha kumrudisha benchi kipa Vincent Angban kutoka Ivory Coast.
    Bado Manyika ana kazi ya kufanya ili kuimarisha kiwango chake zaidi, hatimaye siyo tu kuendelea kuwa ‘Simba One’ bali kufufua na ndoto za siku moja kuwa kipa namba moja wa timu ya taifa, Taifa Stars. 
    Manyika alisajiliwa msimu uliopita kama kipa wa kikosi cha pili na kipa wa tatu wa kikosi cha kwanza, lakini kuumia kwa wakati mmoja kwa waliokuwa makipa wa kwanza (Ivo Mapunda) na wa pili (Hussein Sharrif) wakati huo, kulimfanya aanze kudaka mapema.
    Alidaka mechi za kirafiki katika kambi ya Afrika Kusini kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu, Yanga SC ambao alisimama langoni kwa dakika 90 akidaka kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu bila kufungwa.
    Ulikuwa mwanzo mzuri kwa Manyika, ambaye hakuna shaka anafuata vyema nyayo za baba yake alikuwa 'Tanzania One' kati ya mwaka 1998 na 2000.
    Hata hivyo, baadaye Manyika alianza kufungwa mabao rahisi kiasi cha kuwekwa benchi, lakini sasa amefufua makali yake langoni.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PETER MANYIKA AFIKISHA MECHI 19 ZA KUDAKA BILA KURUHUSU BAO TANGU ATUE SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top