• HABARI MPYA

  Saturday, January 09, 2016

  BOSSOU WA YANGA ‘AMPOTEZA’ WAWA WA AZAM FC, SASA AMFUKUZIA JUUKO WA SIMBA

  MABEKI WA KIGENI NA MABAO YAO TIMU ZA BARA:
  Beki Timu Mabao Mechi
  Serge Wawa Azam FC 0 56
  Juuko Murushid Simba SC 2 41
  Vincent Bossou Yanga SC 1 10
  Beki Mtogo wa Yanga SC, Vincent Bossou amewasuta waliokuwa wanaamini yeye galasa

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  BEKI Mtogo wa Yanga SC, Vincent Bossou amecheza mechi 10 tu hadi sasa tangu ajiunge na mabingwa hao wa Tanzania Bara mwanzoni mwa msimu, lakini tayari amefunga bao moja.
  Maana yake, Bossou amempiku beki raia wa Ivory Coast, Serge Wawa Pascal wa Azam FC, ambaye yuko katika msimu wa pili Tanzania Bara akiwa amecheza mechi 56, lakini hana bao.
  Bossou aliyefunga bao la kusawazisha katika sare ya 1-1 na Azam FC mechi ya Kundi B Kombe la Mapinduzi katikati ya wiki baada ya kutokea benchi kipindi cha pili, sasa anaanza kuifukuzia rekodi ya beki Mganda wa Simba SC, Juuko Murushid.
  Serge Wawa yuko katika msimu wake wa pili Tanzania Bara akiwa amecheza mechi 56, lakini hajafunga hata bao la mkono

  Juuko aliye katika msimu wa pili pia Bara, hadi sasa amecheza mechi 41 na kufunga mabao mawili Msimbazi.
  Tofauti ya Juuko na Wawa, walioanza mara moja kucheza baada ya kusajiliwa, Bossou alilazimika kusubiri hadi Nahodha, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aumie Novemba mwaka jana ili kuanza kucheza.
  Juuko Murushid (kulia) anawazidi Serge Wawa na Bossou idadi ya mabao ya kufunga Tanzania Bara

  Ilifikia wakati hadi waandishi na wachambuzi wa vyombo vya habari wakaanza kuamini Yanga SC imesajili mchezaji galasa, kutokana na Bossou kutopangwa – lakini baada ya kuanza kucheza amebadilisha upepo.
  Sasa wana Yanga SC wanamkubali Bossou kama beki wa kazi ambaye anazimudu hata mechi zinazochafuka, kama ile dhidi ya Azam FC iliyotawaliwa na undava.
  Sasa wana Yanga wanapenda Bossou apangwe kila mechi ngumu, baada ya shughuli alioionyesha ndani ya mechi 10 tu za mwanzo.
  Bossou (kushoto) alilazimika kusugua sana benchi hadi Nadir Haroub 'Cannavaro' alipoumia Novemba
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BOSSOU WA YANGA ‘AMPOTEZA’ WAWA WA AZAM FC, SASA AMFUKUZIA JUUKO WA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top