• HABARI MPYA

  Thursday, January 14, 2016

  LIVERPOOL NA ARSENAL ZAUMIZA NYASI, SARE 3-3, CHELSEA NAYO BADO MWENYE KUSUASUA

  MATOKEO LIGI KUU YA ENGLAND;
  Januari 13, 2016
  Tottenham Hotspur 0 - 1 Leicester City
  Liverpool 3 - 3 Arsenal
  Swansea City 2 - 4 Sunderland
  Manchester City 0 - 0 Everton
  Southampton 2 - 0 Watford
  Stoke City 3 - 1 Norwich City
  Chelsea 2 - 2 West Bromwich Albion
  Januari 12, 2016
  Aston Villa 1 - 0 Crystal Palace
  Bournemouth 1 - 3 West Ham United
  Newcastle United 3 - 3 Manchester United

  Firmino (kulia) akiifungia Liverpool katika sare ya 3-3 na Arsenal jana Uwanja wa Anfield PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  TIMU ya Liverpool imelazimishwa sare ya 3-3 na Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Anfield.
  Roberto Firmino Barbosa de Oliveira aliifungia mabao mawili Liverpool dakika ya 10 na 19, wakati bao lingine lilifungwa na Joe Allen dakika ya 90, huku mabao ya Arsenal yakifungwa na Aaron Ramsey dakika ya 14 na Olivier Giroud mawili dakika ya 25 na 55.
  Pamoja na sare hiyo, Arsenal inaendelea kubaki kileleni ikifikisha pointi 43 baada ya kucheza mechi 21, sasa ikifungana na Leicester City kwa pointi na idadi ya mechi za kucheza.
  Diego Costa akiwa amelala kwenye nyasi baada ya kukosa bao la wazi katika sare ya 2-2 na West Brom jana Uwanja wa Stamford Bridge PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Chelsea nayo jana imelazimishwa sare ya 2-2 na West Bromwich Albion Uwanja wa Stamford Bridge, mabao yake yakifungwa na Cesar Azpilicueta dakika ya 20 na Gareth McAuley aliyejifunga dakika ya 73, huku mabao ya wageni yakifungwa na Craig Gardner dakika ya 33 na 
  James McClean dakika ya 86.
  Manchester City imelazimishwa sare ya 0-0 na Everton Uwanja wa Etihad, wakati Leicester City imefufua tena ndoto za ubingwa baada ya ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspur, bao pekee la Robert Huth dakika ya 83 Uwanja wa White Hart Lane.

  Robert Huth akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Leicester City bao pekee la ushindi dhidi ya Spurs Uwanja wa White Hart Lane jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Sunderland imepata ushindi wa ugenini wa 4-2 dhidi ya Swansea City Uwanja wa Liberty. Mabao ya Sunderland yamefungwa na Jermain Defoe matatu dakika za tatu, 61 na 85 na lingine Patrick van Aanholt dakika ya 49, wakati ya wenyeji yamefungwa na Gylfi Sigurdsson dakika ya 21 kwa penalti na Andre Ayew dakika ya 40.
  Southampton imeshinda 2-0 dhidi ya Watford, mabao ya Shane Long dakika ya 17 na Dusan Tadic dakika ya 73.
  Stoke City imeshinda 3-1 dhidi ya Norwich City, mabao ya Jonathan Walters dakika ya 49, Jose Luis Mato Sanmartin dakika ya 67 na Ryan Bennett aliyejifunga dakika ya 78, huku bao la wageni likifungwa na Jonny Howson dakika ya 55 Uwanja wa Britannia.

  Mshambuliaji wa Manchester City, Raheem Sterling akiangushwa na John Stones wa Everton kwenye eneo la penalti, lakini refa alipeta jambo ambalo lilimkasirisha kocha Manuel Pellegrini  PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL NA ARSENAL ZAUMIZA NYASI, SARE 3-3, CHELSEA NAYO BADO MWENYE KUSUASUA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top