• HABARI MPYA

  Saturday, January 16, 2016

  KIPYENGA CHA KWANZA CHAN 2016 LEO; NI RWANDA NA IVORY COAST

  Rwanda watamenyana na Ivory Coast leo katika mechi ya ufunguzi ya CHAN Uwanja wa Amahoro

  FILIMBI ya kwanza ya michuano ya nne ya Kombe la Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) inatarajiwa kupulizwa leo mjini Kigali, nchini Rwanda.
  Wenyeji, Amavubi wanatarajiwa kufugua dimba kwa kucheza na Ivory Coast Uwanja wa Amahoro, Kigali kuanzia Saa 10:00 jioni katika mchezo wa Kundi A.
  Mchezo huo utafuatiwa na mchezo mwingine wa kundi hilo kati ya Gabon na Morocco utakaoanza Saa 1:00 usiku.
  Kesho mechi za Kundi B zinatarajiwa kuendelea, mabingwa wa kwanza wa michuano hiyo, DRC wakimenyana na Ethiopia Uwanja wa Huye kuanzia Saa 10:00 jioni, kabla ya Angola kumenyana na Cameroon Uwanja wa Huye pia kuanzia Saa 1:00 usiku.
  Rwanda inakuwa nchi ya nne kupewa uenyeji wa michuano hiyo inayoshirikisha wachezaji wanaocheza Ligi za nchini mwao pekee baada ya Ivory Coast mwaka 2009, Sudan 2011 na Afrika Kusini mwaka juzi.
  Bingwa wa kwanza wa michuano hiyo inayozidi kupata msisimko kila mwaka alikuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), aliyefuatiwa na Tunisia na baadaye Libya.

  MAKUNDI CHAN 2016;
  Kundi A; Gabon, Ivory Coast, Morocco na Rwanda
  Kundi B; Angola, Cameroon, DRC na Ethiopia
  Kundi C; Guinea, Niger, Nigeria na Tunisia
  Kundi D; Mali, Uganda, Zambia na Zimbabwe

  RATIBA KOMBE LA CHAN 2016 RWANDA
  Januari 16, 2016
  Rwanda Vs Ivory Coast (Amahoro, Saa 10:00 jioni)
  Gabon Vs Morocco (Amahoro, Saa 1:00 usiku)
  Januari 17, 2016
  DRC Vs Ethiopia (Huye, Saa 10:00 jioni)
  Angola Vs Cameroon (Huye, Saa 1:00 usiku)
  Januari 18, 2016
  Tunisia Vs Guinea  (Nyamirambo, Saa 10:00 jioni)
  Nigeria Vs Niger (Nyamirambo, Saa 1:00 usiku)
  Januari 19, 2016
  Zimbabwe Vs Zambia (Rubavu, Saa 10:00 jioni)
  Mali Vs Uganda (Rubavu, Saa 1:00 usiku)
  Januari 20, 2016
  Rwanda Vs Gabon (Amahoro, Saa 10:00 jioni)
  Morocco Vs Ivory Coast (Amahoro, Saa 1:00 usiku) 
  Januari 21, 2016
  DRC Vs Angola (Huye, Saa 10:00 jioni)
  Cameroon Vs Ethiopia (Huye, Saa 1:00 usiku)
  Januari 22, 2016
  Tunisia Vs Nigeria (Nyamirambo, Saa 10:00 jioni)
  Niger Vs Guinea (Nyamirambo, Saa 1:00 usiku)
  Januari 23, 2016
  Zimbabwe Vs Mali (Rubavu, Saa 10:00 jioni)
  Uganda Vs Zambia (Rubavu, Saa 1:00 usiku)
  Januari 24, 2016
  Morocco Vs Rwanda (Amahoro, Saa 11:00 jioni)
  Ivory Coast Vs Gabon (Huye, Saa 11:00 jioni)
  Januari 25, 2016
  Ethiopia Vs Angola (Amahoro, Saa 11:00 jioni)
  Cameroon Vs DRC (Huye, Saa 11:00 jioni)
  Januari 26, 2016
  Guinea Vs Nigeria (Rubavu, Saa 11:00 jioni)
  Niger Vs Tunisia (Nyamirambo, Saa 11:00 jioni)
  Januari 27, 2016
  Zambia Vs Mali (Nyamirambo, Saa 11:00 jioni)
  Uganda Vs Zimbabwe (Amahoro, Saa 11:00 jioni)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPYENGA CHA KWANZA CHAN 2016 LEO; NI RWANDA NA IVORY COAST Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top