• HABARI MPYA

  Wednesday, January 13, 2016

  KILA LA HERI MTIBWA SUGAR...NA 'MLIMBWENDE' AENDE MANUNGU

  Na Prince Akbar, ZANZIBAR
  MTIBWA Sugar wataniwa Kombe la Mapinduzi dhidi ya URA ya Uganda usiku wa leo, Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Na kocha Mecky Mexime wa Mtibwa Sugar, ambayo imeingia Fainali baada ya kuwatoa waliokuwa mabingwa watetezi, Simba SC Jumapili kwa kuwafunga 1-0 amesema hana wasiwasi na mechi hiyo.
  Mexime, Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kwamba URA ni timu nzuri, lakini wamejipanga kupambana nayo ili wachukue Kombe.
  Mexime amesema anawaamini vijana wake kwamba wana uwezo wa kuifunga URA usiku wa leo katika mchezo ambao utahudhuriwa na Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika, Mbwana Ally Samatta.  
  Ikumbukwe URA imefika katika mechi ya mwisho ya Kombe la Mapinduzi, baada ya kuwatoa mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.
  Hii itakuwa mara ya tano kwa Mtibwa Sugar kufika fainali, baada ya awali kucheza fainali nne na kutwaa taji mara moja, 2010 ilipoifunga Ocean View ya hapa.
  Mtibwa iliingia fainali mwaka 2007 na kufungwa na Yanga SC – wakati 2008 na 2015 ilifungwa na Simba SC mara zote.
  URA ambao wanacheza mashindano haya kwa mara ya pili, hawajawahi kufika fainali, lakini mwaka 2014 taji la Mapinduzi lilipanda ndege kwenda Uganda, lilipochukuliwa na KCCA walioifunga Simba SC katika fainali. Kila la heri Mtibwa Sugar.
  Kikosi cha Mtibwa Sugar kinachopewa nafasi kubwa ya kubeba Kombe la Mapinduzi

  ORODHA YA MABINGWA KOMBE LA MAPINDUZI
  Mwaka            Bingwa Mshindi wa Pili
  2007 Yanga SC Mtibwa Sugar 
  2008 Simba SC Mtibwa Sugar
  2009 Miembeni          KMKM
  2010 Mtibwa Sugar   Ocean View
  2011 Simba SC   Yanga SC
  2012 Azam FC          Simba SC
  2013 Azam FC   Tusker FC
  2014 KCCA       Simba SC
  2015 Simba SC Mtibwa Sugar
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KILA LA HERI MTIBWA SUGAR...NA 'MLIMBWENDE' AENDE MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top