• HABARI MPYA

  Saturday, September 14, 2019

  TANZANIA YAPANGWA KUNDI B PAMOJA NA KENYA, ETHIOPIA NA ZANZIBAR CECAFA CHALLENGE U20

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TANZANIA Bara imepangwa Kundi B pamoja na Kenya, Ethiopia na Zanzibar katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge U20) inayotarajiwa kuanza Septemba 21 hadi Oktoba 5 mjini Kampala, Uganda.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano uliofanyika hoteli ya Imperial Royale mjini Kampala, Uganda Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye amesema kwamba Kundi A litakuwa na wenyeji, Uganda, Sudan, Eritrea na Djibouti.
  Musonye amesema Kundi litazikutanisha timu za Burundi, Sudan Kusini Somali – maana yake nchi wanachama wa CECAFA watakaokosekana kwenye michuano hii ni Rwanda pekee. 

  Wachezaji wa Ngorongoro Heroes wakiwa mazoezini kujiandaa na michuano ya CECAFA Challenge U20

  Ngorongoro Heroes inayofundishwa na kocha Zubery Katwila itafungua dimba na Ethiopia Septemba 22, kabla ya kumenyana na Kenya Septemba 24 na kumaliza mechi zake za Kundi B kwa kupambana na ndugu zao, Zanzibar Septemba 26.
  Hatua ya Robo Fainali itafuatia Septemba 29, Nusu Fainali Okatoba 2 na Fainali ya michuano ya CECAFA Challenge U20 mwaka 2019 itapigwa Oktoba 5.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA YAPANGWA KUNDI B PAMOJA NA KENYA, ETHIOPIA NA ZANZIBAR CECAFA CHALLENGE U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top