• HABARI MPYA

  Wednesday, September 11, 2019

  MAKA EDWARD WA YANGA ASAINI MINNE KUJIUNGA NA KLABU YA LIGI KUU MOROCCO

  Na Saada Salim, DAR ES SALAAM
  KIUNGO chipukizi Mtanzajia, Maka Edward Mwasomola amesaini mkataba wa miaka minne kujiunga na klabu ya Moghreb Athletic de Tetouan inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco.
  Maka ambaye kwa misimu mitatu iliyopita alikuwa na klabu ya Yanga baada ya kupandishwa kutoka kikosi cha vijana na wakati wote huo amekuwa akiitwa timu mbalimbali za vijana.
  Baada ya msimu uliopita aliomba kutosajiliwa Yanga SC kwa sababu ya mipango yake ya kwenda nje kucheza soka ya kulipwa, yeye pamoja chipukizi wengine wawili, beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na mshambuliaji, Yohana Oscar Mkomola.

  Maka Edward amesaini mkataba wa miaka minne kujiunga na Moghreb Tetouan ya Ligi Kuu Morocco

  Nkomola amejiunga na kikosi cha pili cha Vorskla Poltava II ya Ukraine, wakati Ninja amejiunga na kikosi cha pili pia cha LA Galaxy II kwa mkopo kutoka MFK Vyskov ya Czech.  
  Moghreb Athlétic de Tetouan, kwa kifupi MA Tetouan ni klabu yenye maskani yake Tetouan na ilianzishwa mwaka 1956 na iliwahi kushiriki ligi za Hispania kwa jina la Athletic Club Tetuan kuanzia mwaka 1922 hadi 1947 na Club Atletico de Tetuan kati ya 1947 na 1956 hadi mwaka 1956 Morocco ilipopata Uhuru wake kutoka Hispania. 
  Klabu hiyo ikaanza kushiriki Ligi ya Morocco baada ya mfarakano uliozalisha timu mbili, nyingine AD Ceuta FC iliyobaki Hispania.
  Maka anakuwa mchezaji wa tatu wa Tanzania kucheza Morocco, baada ya beki chipukizi Nickson Kibabage kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro na kiungo mshambuliaji Simon Happygod Msuva kutoka Yanga opia, ambao wote wanachezea Difaa Hassan El-Jadidi ya Ligi Kuu pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAKA EDWARD WA YANGA ASAINI MINNE KUJIUNGA NA KLABU YA LIGI KUU MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top