• HABARI MPYA

    Saturday, February 02, 2019

    TFF YAZUNGUMZA NA VODACOM CHINI YA USIMAMIZI WA SERIKALI WARUDI LIGI KUU

    Na Mwandishi Wetu, ARUSHA
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema kwamba wameanza tena mazungumzo na Kampuni ya Vodacom ili irejeshe udhamini katika Ligi Kuu ya Bara.
    Karia ameyasema hayo leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC) mjini Arusha wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa TFF.  
    Karia amesema siyo kwamba Vodacom walijitoa kudhamini ligi, bali kiasi walichotaka kutoa kilikuwa hakikidhi, hivyo, TFF ikakataa kuingia makubaliano hayo, kwani wangesaini mkataba huo wangeonekana wajinga.

    Rais wa TFF, Wallace Karia amesema wameanza tena mazungumzo na Vodacom ili irejeshe udhaminiLigi Kuu 

    “Hata kama ni masikini basi usikubali makubaliano ambayo hayana tija" amesema Karia na kuongeza kwamba kwa sasa wanaendelea na mazungumzo na Vodacom chini ya usimamizi wa Serikali.
    Mkutano Mkuu wa TFF pia umefanya uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji akiwakilisha Kanda ya Shinyanga na Simiyu ambapo Osuri Charles Kosori ameshinda kwa kura 91 akiwapiku Benister Rugora aliyepata kura 20 na Kanjanja Magesa aliyepata kura 17.
    Katika mkutano huo, Karia aliwaapisha wajumbe wapya wa kamati ya utendaji ambao ni Ahmed Iddi ‘Msafiri’ Mgoyi na Athumani Nyamlani ambao aliwateua.
    Mwingine aliyeapishwa ni Stephen Mguto ambaye anakuwa Mjumbe wa Kamati hiyo kutokana na nafasi yake ya kuwa Uenyekiti wa Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAZUNGUMZA NA VODACOM CHINI YA USIMAMIZI WA SERIKALI WARUDI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top