• HABARI MPYA

  Friday, June 01, 2018

  MTIBWA SUGAR, HASSAN DILUNGA WAINGIA KATIKA MAZUNGUMZO YA MKATABA MPYA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Mtibwa Sugar ipo kwenye mazungumzo na kiungo Hassan Dilunga ili kumuongezea mkataba aendelee kufanya kazi Manungu.
  Mkurugenzi wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser amesema kwamba baada ya msimu mzuri huu unaofikia tamati kesho wataanza mazungumzo na Dilunga juu ya kumuongezea mkataba.
  Bayser amesema kwamba amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na wanataka wampe mkataba mrefu wa kumfanya adumu Manungu kwa muda mrefu na kuboreshewa maslahi.

  Hassan Dilunga anaingia kwenye mazungumzo ya mkataba mpya na Mtibwa Sugar

  “Dilunga ni mchezaji wa Mtibwa Sugar, kwa sasa ana mkataba wa mwaka mmoja zaidi, lakini wiki ijayo tutaanza mazungumzo nao juu ya mkataba mpya,”amesema Dilunga.
  Pamoja na hayo, Bayser amesema kwamba Mtibwa Sugar itaendelea na sera zake za kuibua wachezaji vijana kutoka kwenye akademi yake.
  Mtibwa Sugar wanakamilisha msimu wa soka nchini kesho kwa mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanazania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Singida United Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
  Na Dilunga akiwa katika ubora wa hali ya juu msimu huu, anatarajiwa sana kuwa chachu ya ushindi wa Mtibwa Sugar kesho Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR, HASSAN DILUNGA WAINGIA KATIKA MAZUNGUMZO YA MKATABA MPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top