• HABARI MPYA

    Tuesday, June 19, 2018

    WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI WAWAKATALIA VIONGOZI ZFA TAIFA KUJIUZULU

    Na Abdi Suleiman, PEMBA
    HATIMAE wajumbe kamati Tendaji ya chama cha soka Zanzibar ZFA Taifa, wamezikataa barua za kujiuzulu kwa viongozi wa juu wa Chama.
    Wajumbe wa kamati hiyo waliokutana tarehe 18, mwezi huu katika ofisi ya ZFA Chakechake Pemba, huku kikao hicho kikiongozwa na Mwenyekiti wake Sharif Juma Said.
    Akizungumza na waandishi wa habari za Michezo Pemba, Mwenyekiti huyo alisema, wajumbe wamezikataa barua za viongozi hao wa juu, kwa lengo la kuepuka kadhia ambayo inayoweza kuipata hapo mbele, kutokana na timu za Zanzibar zinatarajiwa kushiriki mashindano mbali mbali ya kimataifa.

    Alisema awali kabla ya kuanza kikao hicho, walianza kwa kupitia vifungu mbali mbali vya katiba ya ZFA ya mwaka 2010, ikiwemo kupata idadi ya wajumbe wa upande wa Pemba.
    Alisema, Pemba inawajumbe 14, na waliohudhuria katika kikao hicho ni wajumbe 13, huku wakitumia kifungu cha 12 katika katiba hiyo ili kupata maamuzi na kikao cha ZFA, pamoja na kusema kikao hicho kimepata baraka kutoka kifungu cha 12:2(ii) na kuwa halali.
    “Kilichotuleta hapa ni kupitia barua ya Makamu wa Rais wa ZFA Pemba Ali Mohamed Ali, aliyowasiliza ZFA juu ya kujuuzulu kwake Juni 13 mwaka huu,”alisema.
    Mwenyekiti huyo alisema baada ya kuipitia barua hiyo kwa mujibu wa katiba ya ZFA suara ya 12 kifungu cha 92 kimesema ‘bila ya kujali sababu yoyote, mjumbe yoyote anayohaki ya kujiuzulu katika wadhifa alionao’, 92:1 kimesema mjumbe hatajiuzulu mpaka apeleke kwa kamati tendaji katika ngazi inayohusika, ndipo kifungu cha 92:2 ndicho kilichowapa nafasi ya kusikiliza ombi la mjumbe.
    “Sisi hapa hatukaja kujadili bali tumekuja kukubali ombi lake au kukataa ombi lake, la kujiuzulu wadhifa wake tu,”alisema.
    Aidha alisema baada ya kufikia muwafaka, wajumbe walitumia kifungu cha 36 katika katiba ya mwaka 2010 ya ZFA, juu ya upigaji wa kura, ili kufikia maamuzi ambapo maamuzi yanaweza kufikiwa kwa njia ya upigaji wa kura, (i) upigaji wa kura utakuwa wa siri kwa kamati tendaji (ii) maamuzi yaweze kuafikiwa na wajumbe.
    Alisema upigaji wa kura hizo wajumbe 13 waliohudhuria kikao hicho, kura mbili ziliharibika na kura tano zimkukubali kujiuzulu kwa makamu huyo wa Rais wa ZFA, huku kura sita ziliweza kumkatalia maamuzi yake ya kujuuzulu wadhifa huo na wajumbe kumtaka katibu wa ZFA Taifa, kumuandikia barua ya kurudi tena katika nafasi yake ya uongozi.
    “Kutokana na maamuzi hayo ya wajumbe ya upigaji wa kura, kikao hicho hakikuridhia kujiuzulu kwa makamo huyo,” huku wakimtaka katibu Mkuu kumuandikia barua ikizingatiwa mbele kuna hatua ya nane bora ya ligi kuu ya Zanizbar.
    Wakati huo huo alisema Kamati hiyo ilikaa kikao Juni 12 ambapo wajumbe walikuwa 10 na kutimiza matakwa ya sheria, kwa kupitia barua mbili, ikiwemo ya kujiuzulu kwa Rais wa ZAF Ravia Idarous Faina na Mkurugenzi wa Ufundi Abdullghan Msoma ambayo ilikwenda kwa Rais.
    Alisema kura 10 ziliweza kumkatalia kujiuzulu kwa Ravia na kumtaka katibu mkuu kumuandikia barua ya kurudi madarakani, huku Mzee Zam Ali akiridhiwa kujiuzulu kwake kutokana na sababu mbali mbali alizozieleza katika barua yake.
    Kumbuka kujiuzulu kwa viongozi hao wa ZFA kunatokana na timu ya Karume boys kuondolewa kwenye mashindano makubwa hivi karibuni, kwa kupeleka wachezaji wenye umri mkubwa, ijapokuwa umri unaotakiwa ulitumwa kwa ZFA.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI WAWAKATALIA VIONGOZI ZFA TAIFA KUJIUZULU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top