• HABARI MPYA

    Wednesday, June 27, 2018

    BANDA APANIA KUONGEZA BIDII BAROKA FC AFANYE MAKUBWA ZAIDI AFRIKA KUSINI MSIMU UJAO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BEKI wa kimataifa nchini, Abdi Hassan Banda amesema kwamba wachezaji wamekubaliana kuongeza bidii msimu ujao timu yao, Baroka FC ifanye vizuri nchini Afrika Kusini.
    Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online kwa simu kutoka mabao makuu ya timu hiyo, Ga-Mphahlele jirani kabisa Polokwane, Limpopo Banda amesema kwamba baada ya wachezaji kukutana kuanza maandalizi ya msimu mpya wamekubaliana kupigania matokeo mazuri.
    “Sisi wenyewe tumejitathmini na kugundua tulikuwa bora kuliko timu nyingi, pamoja na kulia na bahati, lakini tumekubaliana tuongeze bidii msimu ujao tupate matokeo mazuri,”amesema Banda.  
    Banda anaingia katika msimu wake wa pili Baroka FC tangu asajiliwe kutoka Simba SC ya Dar es Salaam Julai mwaka jana (2017), alikocheza kwa misimu mitatu baada ya kuwasili akitokea Coastal Union ya kwao mkoani Tanga.
    Abdi Banda akiwa mazoezini wachezaji wenzake Baroka FC juzi baada ya kukutana kwa maandalizi ya msimu mpya


    Mume huyo mtarajiwa wa Zabib Kiba, dada wa mwanamuziki Ali KIba hakuwa na msimu mzuri sana wa kwanza Baroka FC, kwani timu hiyo ilinusurika kushuka daraja baada ya kushika nafasi ya mwisho kufuatia timu mbili, Platinum Stars na Ajax Cape Town kuteremka, ikimaliza na pointi 34 katika mechi 30.
    Lakini wengi miongoni mwa wataalamu wa soka, wakiwemo wachambuzi na makocha wameridhika msimu mmoja wa kucheza Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini umembadilisha Banda kiuchezaji na sasa amekuwa beki bora zaidi.
    Miongoni mwa wanaoridhishwa na uchezaji wa beki huyo kwa sasa ni kocha Jamhuri Kihwelo wa Dodoma FC, ambaye alicheza na baba yake Abdi, Hassan Banda katika katika klabu ya Simba, ambaye naye alikuwa beki wa kati na kiungo wa ulinzi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BANDA APANIA KUONGEZA BIDII BAROKA FC AFANYE MAKUBWA ZAIDI AFRIKA KUSINI MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top